Theology of the Church, Swahili Student Workbook
4 0 /
THEOLOJIA YA KANISA
nyoka. Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu. Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.» Chukukulia mfano wa mhubiri kijana ambaye amegundua kuwa mahubiri yake mengi yanatoka katika Maandiko ya Agano Jipya. Anakiri, “Sielewi jinsi vita, amri, na hadithi za Agano la Kale zinavyohusiana na kusanyiko langu la kanisa.” Je, unaweza kumsaidiaje aelewe kwamba historia ya watu wa Mungu wa Agano la Kale (Israeli) ni msingi wa kuelewa kile ambacho Mungu anafanya kwa watu wake wa Agano Jipya (Kanisa)? Je, kufikiria Kanisa kama «watu wa Mungu» kunatusaidiaje katika kuunganisha jambo hili? Wakati wakiwashirikisha majirani zao kuhusu imani yao, kundi la vijana lilifika kwenye nyumba ambamo wenyeji walikuwa waamini, lakini walibishana na wahudumu hao vijana wakiwaambia kwamba kanisa ambalo vijana hao walihudhuria halikuwa bora. “Kuna desturi nyingi ambazo ninyi mnashiriki ambazo zilianza katika mataifa ya kipagani – Krismasi, Pasaka ( Easter ), na hasa masuala ambayo kanisa lenu linaruhusu – muziki wa rock, kwenda sinema, kucheza, na mambo mengine ambayo yanaonyesha kuwa ninyi sio watakatifu!” Waliposikia hayo, baadhi ya vijana walikata tamaa sana, na wengine hata walifikiri kwamba wao si Wakristo kweli. Mchungaji wa vijana anataka kuwafundisha wanafunzi wake kuhusu asili ya neema ya Mungu na umoja na Kristo, bila kuonekana kana kwamba anapingana na waamini wale ambao vijana walikutana nao. Aseme nini kuhusu Kanisa ili kufafanua tatizo hili la kanisa lipi na kusanyiko lipi ni bora? Wokovu wa Kikristo unamaanisha kwamba mtu ameokolewa kutoka katika hali ya kupotea na kutengwa na Mungu ambayo ilisababishwa na dhambi, kwa kuunganishwa na Kristo na hivyo kuwa sehemu ya “watu wa Mungu” ambao wanarithi Ufalme aliouahidi. Kanisa la Yesu Kristo lilifunuliwa kwa namna ya kivuli kupitia utekelezaji wa Mungu wa kusudi lake kuu, yaani, Mungu aliamua karne nyingi zilizopita kujitukuza mwenyewe kwa kuokoa jamii mpya ya wanadamu kupitia agano ambalo Mungu aliliweka na Ibrahimu. Nia hii ni sehemu muhimu ya ufunuo unaoendelea wa mpango wake wenye neema wa wokovu, yaani, siri kuu ya ujumuishwaji wa mataifa katika Kristo Yesu. Kupitia watu wa Israeli, Mungu ametupatia picha ya watu wake wa kipekee, laos wa Mungu, Kanisa, kama linavyomwakilisha Mungu na Ufalme wake leo. “Kanisa Letu ndilo Kanisa Sahihi.”
1
4
Marudio ya Tasnifu ya Somo
Made with FlippingBook flipbook maker