Theology of the Church, Swahili Student Workbook

/ 4 1

THEOLOJIA YA KANISA

Iwapo unavutiwa kufuatilia baadhi ya mawazo kuhusu Ufunuo Kivuli wa Kanisa katika Mpango wa Mungu , unaweza kujaribu kusoma vitabu vifuatavyo: Sura ya 6 katika kitabu cha Fee, Gordon D. Paul, the Spirit, and the People of God. Peabody, MA: Hendrickson Publishers, 1996. Snyder, Howard A. Kingdom, Church, and World: Biblical Themes for Today . Eugene, OR: Wipf and Stock Publishers, 2001. -----. The Problem of Wineskins: Church Structure in a Technological Age. Downers Grove: InterVarsity, 1975. Wallis, Jim. Agenda for Biblical People. New York: Harper and Row, 1976. Sasa ni wakati wa kujaribu kukazia theolojia hii ya kiwango cha juu kwa kuiweka katika vitendo kupitia mazingira fulani halisi ya huduma, ambayo utayafikiria na kuyaombea wakati wote wa juma lijalo. Ni kitu gani hasa ambacho Roho Mtakatifu anakuelekeza kuhusu wazo la Kanisa kufunuliwa awali katika agano la Mungu na Ibrahimu, pamoja na ufunuo wa siri ya ushiriki wa mataifa katika wokovu? Ni hali gani maalum inayokuja akilini mwako unapofikiria kuhusu uhusiano kati ya imani binafsi katika Yesu na katika mwili wa Kristo? Je, unaweza vipi kibinafsi kutimiza kweli ya fundisho la kwamba kuwa umoja na Kristo ni kuwa umoja na watu wake? Je, kuna watu ambao wanahitaji kusikia ukweli huu kwa mara ya kwanza, au watu ambao wanahitaji kufafanuliwa zaidi sasa hivi? Tenga muda wa kutafakari kuhusu hali yako binafsi ya maisha na huduma, na omba Roho Mtakatifu akuletee watu au hali zinazofaa akilini mwako kwa ajili ya kutekeleza kweli hizi na kanuni hizi. Ili kuielewa vyema nafasi na umuhimu wa Kanisa katika mpango wa Mungu, tunahitaji mafundisho na uongozi wa Roho Mtakatifu. Paulo alisema kwamba ufunuo wa siri ya mataifa kuwa sehemu ya familia ya Mungu uliletwa kupitia mafundisho ya Mungu kupitia manabii na mitume (taz. Rum. 16:25-27; Efe. 3:3- ). Ni Mungu Roho Mtakatifu pekee ndiye anayeweza kutufundisha jinsi watu wa Mungu wanavyopendwa na Kristo na walivyo wa thamani kwake, na jinsi ilivyo muhimu kwetu kujitoa kuwatumikia na kuwajenga watu wa Mungu. Muombe Mungu akusamehe ikiwa umekuwa na mawazo duni au yasiyostahili kuhusu Kanisa. Muombe akuonyeshe kwa upya nafasi ya Kanisa katika shughuli za ufalme wake, na muombe akupe nguvu mpya, hekima na rasilimali unapomtumikia kwa kuwatumikia watu wake.

Nyenzo na Bibliografia

1

Kuhusianisha Somo na Huduma

Ushauri na Maombi

Made with FlippingBook flipbook maker