Theology of the Church, Swahili Student Workbook

4 2 /

THEOLOJIA YA KANISA

MAZOEZI

1 Petro 2:9-10

Kukariri Maandiko

Ili kujiandaa kwa darasa, tafadhali tembelea www.tumi.org/books ili kupata kazi ya usomjai ya wiki ijayo, au muulize mkufunzi wako.

Kazi ya Usomaji

Kazi yako inaanza kwa dhati kwa somo linalofuata, hivyo usichelewe au kutafuta kujifunza kwa haraka mwishoni. Jipe muda wa kutosha kuzingatia kusoma ili uweze kuelewa dhana zitakazojadiliwa wiki ijayo. Aidha, endelea na kazi yako ya kukariri Maandiko, na kupitia kwa umakini mambo uliyojifunza juma hili kwa ajili ya maandalizi ya mtihani wako ujao. Zingatia kwamba mtihani wako kipindi kijacho utalenga hasa yaliyomo kwenye video na muhtasari uliojadiliwa katika somo hili . Hivyo, hakikisha unatumia muda wako kupitia kumbukumbu zako, ukiangazia hasa mawazo makuu ya somo. Tafadhali soma maeneo ya vitabu ulivyoelekezwa kusoma na uandike muhtasari wa kila eneo la usomaji usiozidi aya moja au mbili kwa kila eneo moja. Andika muhtasari wako kwa ufupi na kwa namna rahisi; katika muhtasari wako, eleza ufahamu wako bora wa kile unachofikiria kilikuwa kiini cha kila moja ya maeneo ya usomaji. Usijali sana kuhusu kutoa maelezo mengi, bali andika kile unachokiona kama wazo kuu lililojadiliwa katika sehemu hiyo ya kitabu. Tafadhali leta muhtasari husika darasani wiki ijayo. (Tafadhali angalia “Fomu ya Ripoti ya Usomaji” mwishoni mwa somo hili). Katika somo hili, tulizungumzia kuhusu mpango wa milele wa Mungu wa kuita watu kutoka duniani kote kwa ajili yake, ambao wataishi milele pamoja naye katika Yerusalemu Mpya. Katika somo linalofuata, tutazungumzia kuhusu neema ya Mungu inayowawezesha wenye dhambi kuwa sehemu ya watu wake walioteuliwa, na jinsi neema hiyo inavyotufanya tuitikie kwa ibada na sifa. Somo linalofuata, kimsingi, linaitwa “Kanisa Katika Ibada” na linatufundisha kuwa moja ya sababu muhimu zaidi za kuwepo kwa Kanisa ni kumpa Mungu utukufu Anaostahili!

Kazi Zingine

1

Kuelekea Somo Linalofuata

Mtaala huu ni matokeo ya maelfu ya masaa ya kazi iliyofanywa na taasisi ya The Urban Ministry Institute (TUMI) na haupaswi kudurufu bila idhini ya taasisi hiyo. TUMI inatoa idhini kwa yeyote anayehitaji kutumia vitabu hivi kwa ajili ya faida ya ufalme wa Mungu, kwa kutoa leseni za kudurufu za gharama nafuu. Tafadhali thibitisha kwa Mkufunzi wako ikiwa kitabu hiki kimepewa leseni ipasavyo. Kwa taarifa zaidi kuhusu TUMI na taratibu zetu za utoaji leseni, tembelea www.tumi.org na www.tumi.org/license .

Made with FlippingBook flipbook maker