Theology of the Church, Swahili Student Workbook
4 6 /
THEOLOJIA YA KANISA
kwa Mungu kwa baraka zake kuu katika kusimamishwa kwa nyumba yake (2 Nya. 7:5). Kinachoshangaza sana ni kwamba hakuna mtu aliyepaswa kuja mbele za uwepo wa Mungu bila kumtolea kitu cha kutolewa dhabihu kwa niaba yake. Mungu anastahili matoleo yetu yaliyo bora zaidi, ya juu zaidi, na ya muhimu zaidi, na zaidi hata ya zawadi zetu na vitu vyetu, anastahili nafsi zetu wenyewe. Tunapaswa kumtolea sifa zetu kuu kabisa, sio tu katika nyakati tunapoburudishwa na kuwa na uwezo zaidi, bali hata katika nyakati za magumu na majaribu makubwa zaidi. Mungu wetu hawezi kubadilika; anastahili kuabudiwa pasipo kujali vyovyote mambo yanavyoenda katika maisha na huduma zetu. Ameinuliwa juu ya viumbe vyote, yeye ni Bwana Mungu, anayestahili nguvu zetu, nyimbo zetu bora zaidi, kucheza kwetu kwa kupendeza zaidi, huduma yetu kuu zaidi, mwitikio wetu wa nguvu zaidi. Kanisa katika Ibada daima humtolea Mungu dhabihu inayolingana na utakatifu wake na inayostahili kutambulika kwake. Kwa kweli anastahili kuabudiwa, kupewa sifa zetu. Nabii Habakuki anatuangazia njia katika suala la kumtolea Mungu dhabihu ya sifa: Hab. 3:17-19 – Hata kama mitini isipochanua maua, wala mizabibu kuzaa zabibu; hata kama mizeituni isipozaa zeituni, na mashamba yasipotoa chakula; hata kama kondoo wakitoweka zizini, na mifugo kukosekana mazizini, 18 mimi nitaendelea kumfurahia Mwenyezi – Mungu nitamshangilia Mungu anayeniokoa. 19 Bwana, Mwenyezi – Mungu ndiye nguvu yangu, huiimarisha miguu yangu kama ya paa, huniwezesha kupita juu milimani. Hebu na tusikilize maneno ya mwandishi kwa Waebrania: Eb. 13:15 – Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamayo jina lake. Baada ya kukiri na/au kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (iliyopo kwenye viambatisho), omba maombi yafuatayo: Mungu wa Milele, Baba yetu, Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Wewe peke yako unastahili sifa zote, na kwa sababu hiyo, unahitaji kwamba tukupe heshima na utukufu na sifa. Tunakukaribia kwa jina la Mwanao mpendwa na Mwokozi wetu Yesu Kristo, tukiomba kwamba utujalie nguvu za Roho ili kukutukuza kwa mioyo yetu yote katika ibada ya furaha kwenye mikutano yetu yote, katika mahusiano yetu yote, katika matendo yetu yote, na katika huduma zetu zote. Pokea yote tunayosema na kufanya kama dhabihu inayokubalika ambayo tunaitoa kwako kama Bwana Mungu wetu, ustahiliye sifa na utukufu, katika jina la Yesu tunaomba, Amina.
2
Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi
Made with FlippingBook flipbook maker