Theology of the Church, Swahili Student Workbook

/ 4 7

THEOLOJIA YA KANISA

Weka kando daftari lako na nyenzo za kujifunzia, kusanya pamoja mawazo na tafakuri zako, kisha ufanye Jaribio la Somo la 1, Ufunuo Kivuli wa Kanisa katika Mpango wa Mungu.

Jaribio

Mazoezi ya Kukariri Maandiko

Pitia pamoja na mwanafunzi mwenzako, andika na/au nukuu andiko la kukumbuka la kipindi kilichopita: 1 Petro 2:9-10.

Kusanya muhtasari wako wa kazi ya usomaji ya wiki iliyopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache kuhusu mambo muhimu uliyoyaona katika vitabu ulivyoelekezwa kusoma, yani hoja kuu ambazo waandishi walitaka kuziwasilisha (taz. Fomu ya Ripoti ya Usomaji).

Kazi za Kukabidhi

2

MIFANO YA REJEA

Neema

Nilisikia hadithi kuhusu mtu ambaye alikuwa akifanya majaribio yahusuyo tabia ya mwanadamu. Mtu huyu alisimama karibu na pampu kwenye kituo cha mafuta katika jiji kubwa na kujaribu kugawa noti za dola ishirini kwa watu waliofika kwenye kituo hicho. Ilimshangaza kuona kwamba hakuna mtu ambaye alichukua zile pesa. Pengine sisi tunaoishi mijini hatushangazwi sana na mwitikio huo. Watu wengi katika majiji makubwa wamejifunza kwa uchungu kwamba “hupati kitu bure” na kwamba mtu yeyote anayeonekana kutoa kitu cha thamani bila malipo huenda si wa kuaminiwa. Sisi wakazi wa mijini tunafahamu kwamba ikiwa kitu kinaonekana kuwa kizuri sana pasipo kasoro ndani yake, basi liko jambo fulani ambalo haliko sawa. Ni kawaida kwetu kuwa na mashaka na vitu vya bure. Somo la leo linahusu ibada kama mwitikio wa neema ya Mungu. Injili ni habari njema ya kwamba kila kitu tunachohitaji na tusingeweza kuwa nacho kinatolewa kwetu na Mungu kama zawadi ya bure ya neema. Kama watu wale kwenye kituo cha mafuta, pengine wengi wetu hatukutambua kwamba neema ya Mungu ni zawadi ya bure kabisa. Ni lini ulitambua kwa mara ya kwanza kwamba zawadi ya wokovu kamwe haiwezi kupatikana kwa jitihada binafsi bali inakuja tu kama zawadi inayotakiwa kupokelewa?

1

Kwenda Mbali Kupita Kiasi

Ikiwa kanisa lako lingetakiwa kujibu swali hili, lingejibuje: “Aina zote za ibada na sifa zimeamriwa kuelekezwa kwa Mungu, lakini kusema ukweli, kujihusisha na (X) kwa namna fulani ni kwenda mbali kupita kiasi. ” Je, katika muktadha wa

2

Made with FlippingBook flipbook maker