Theology of the Church, Swahili Student Workbook

5 6 /

THEOLOJIA YA KANISA

C. Ilifanywa mara kwa mara tangu siku za kwanza za Kanisa na kuendelea

Ushahidi wote wa awali. . . ulionyesha kwamba ingawa vipengele vya ibada [ya Kanisa la kwanza] havikuwa na mpangilio maalum, tukio kuu la ibada ya kila juma katika Siku ya Bwana lilikuwa ni sakramenti ya Meza ya Bwana. ~ R. G. Rayburn. “Worship in the Church.” Evangelical Dictionary of Theology. Walter A. Elwell, mh. Grand Rapids: Baker, 1996. uk. 1193. [Meza ya Bwana] ingeweza kuadhimishwa kwa njia inayofaa zaidi, kama ingetolewa kwa Kanisa mara kwa mara, angalau mara moja kwa juma. . . . Inatupasa kila mara kuhakikisha kwamba hakuna mkutano wa Kanisa unaofanywa bila neno, maombi, meza ya Bwana, na [kukusanya pesa kwa ajili ya maskini]. ~ John Calvin. Institutes . 4.17.43-44. Sababu ya pili ya kwa nini kila Mkristo anapaswa [kushiriki ushirika] mara nyingi kadiri awezavyo, ni kwa sababu faida za kufanya hivyo ni kubwa sana. . . . Neema ya Mungu iliyotolewa humo inatuthibitishia msamaha wa dhambi zetu, kwa kutuwezesha kuziacha. Kama miili yetu inavyoimarishwa kwa mkate na divai, ndivyo roho zetu zinavyoimarishwa kwa ishara hizi za mwili na damu ya Kristo. Hiki ndicho chakula cha nafsi zetu: Hutupa nguvu ya kutekeleza wajibu wetu, na hutuongoza kwenye ukamilifu. Kwa hiyo, ikiwa tunajali kwa namna yoyote ile amri iliyo wazi ya Kristo, ikiwa tunataka msamaha wa dhambi zetu, ikiwa tunataka nguvu ya kuamini, kumpenda na kumtii Mungu, basi hatupaswi kupuuza fursa yoyote ya kupokea Meza ya Bwana; basi tusiipe kisogo kamwe karamu ambayo Bwana wetu ametuandalia. Hatupaswi kupuuza tukio lolote ambalo majaliwa mema ya Mungu hutupatia kwa kusudi hili. Hii ndiyo kanuni ya kweli: Tunapaswa kuipokea mara nyingi kadiri Mungu anavyotupa nafasi. Basi mtu ye yote asiyeipokea, bali anatoka katika meza takatifu, wakati vitu vyote vimetayarishwa, ni ama haelewi wajibu huu, au hajali amri ya mwisho ya Mwokozi wake kabla ya kufa, msamaha wa dhambi zake, kuimarishwa kwa nafsi yake, na kuburudishwa kwa tumaini la utukufu. ~ John Wesley. “Sermon 101: The Duty of Constant Communion.” The Works of John Wesley . Toleo la 7-8. uk. 148.

2

Made with FlippingBook flipbook maker