Theology of the Church, Swahili Student Workbook

/ 5 7

THEOLOJIA YA KANISA

D. Chakula cha Bwana kinapaswa kuliwa kwa toba na imani.

1. Sababu mojawapo iliyowafanya wanamatengenezo wa Kiprotestanti kuachana na makanisa ya Kikatoliki kwa mara ya kwanza ni kwa sababu walihisi kwamba sakramenti zilikuwa zikitazamwa kama kitendo cha kiganga badala ya neema ya Mungu iliyopokelewa kwa imani.

2. Meza ya Bwana si kama ibada ya kichawi ambayo hupelekea kutolewa kwa neema kwa kule kushiriki tu katika tendo hilo.

2

Wanamatengenezo wa awali wa Kiprotestanti walipinga fundisho la Kikatoliki ambalo lilijulikana kama ex opere operato . (Hiki ni kifungu cha maneno ya Kilatini kinachomaanisha “kwa msingi wa tendo lililotendwa.”) Hili lilimaanisha kwamba sakramenti iliyotolewa ilileta matokeo yaliyotarajiwa pasipo kujali kama mtu anayeitoa au yule anayeipokea alikuwa akitenda kwa imani. Wanamatengenezo walilipinga hilo na kudai kwamba lilikuwa limefanya watu wazione sakramenti kama uganga au uchawi: kwamba kubatizwa au kula Mlo wa Bwana kulifanya mtu awe Mkristo. Jibu lao lilikuwa kwamba mtu anakuwa Mkristo na kukua kama Mkristo “kwa imani pekee.” Wakatoliki wanaendelea kufundisha ex opere operato isipokuwa wamebadili fundisho lao ili kukazia upya kwamba kupokea sakramenti kwa imani si wazo la Kiprotestanti tu bali ni jambo la lazima kwa maoni ya Kikatoliki vilevile kwa kusema kwamba “[sakramenti] hutangulia imani” na kwamba, “zikiadhimishwa ipasavyo katika imani, sakramenti hutoa neema.” ~ Catechism of the Catholic Church . Liguori, MO:Liguori Publications, 1994. uk. 291-293.

E. Kuna mitazamo minne muhimu ya Kikristo juu ya Meza ya Bwana (ona kiambatisho cha 17).

1. Ubadilishaji ni imani kwamba mkate na divai hugeuka mwili na damu halisi ya Yesu Kristo. Huu ni mtazamo wa Meza ya Bwana unaoshikiliwa na Wakristo wa Kikatoliki.

Made with FlippingBook flipbook maker