Theology of the Church, Swahili Student Workbook
/ 6 5
THEOLOJIA YA KANISA
2. Kanisa linamtukuza Bwana kwa sababu ya wokovu wake wa ajabu, Zab. 103:8-13. Kanisa linasukumwa na shukrani kwa Mungu, kwa ajili ya upendo wake katika Yesu Kristo, na wokovu wenye utukufu ambao ametupa ndani yake.
Kanisa linamwabudu Mungu wa Utatu kwa njia ya Yesu Kristo.
E. Kanisa linamwabudu Mungu peke yake: Mungu wa Utatu – Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ambaye hatashiriki utukufu wake na mwingine yeyote, na Yeye peke yake ndiye anayestahili sifa zetu kuu na bora zaidi.
1. Yesu anatufundisha kwamba Baba anawatafuta watu wake ili wampe aina fulani ya ibada (Yohana 4:21-24).
2
2. Mungu ambaye Kanisa linamwabudu hatashiriki utukufu wake na mwingine.
a. Isa. 48:11
b. Isa. 42:8
c. Yoh. 5:22-23
F. Kanisa humwabudu na kumtukuza Mungu kwa njia ya Yesu Kristo.
1. Damu yake iliyomwagika msalabani inalipa Kanisa nafasi ya kuingia katika uwepo wa Mungu, Ebr. 10:19-20.
2. Damu yake husafisha dhamiri zetu kutokana na matendo mafu ili tumwabudu na kumtumikia Mungu katika kweli na kwa imani, Ebr. 9:13-14.
Made with FlippingBook flipbook maker