Theology of the Church, Swahili Student Workbook

6 8 /

THEOLOJIA YA KANISA

e. Kwa kupiga magoti mbele za Mungu , Zab. 95:6-7a

B. Kupitia liturujia yetu Ufafanuzi: Liturujia = utaratibu maalum wa huduma ambapo tunatangaza Neno la Mungu na kusherehekea pamoja kwenye meza ya Bwana. Tunapochunguza uthibitisho wa ibada ya Kikristo ya Kanisa la kale, tunaona kwamba ilitofautiana na dini za Waroma kwa kuwa haikudai sanamu za ibada, mahekalu, au dhabihu za kawaida. Ilielekezwa katika Neno, kama ilivyohusiana kwa karibu kihistoria na ibada ya Kiyahudi katika sinagogi. Pamoja na hilo, waamini wa kale walikusanyika na kufanya aina fulani za matendo ya kiibada. Waamini walikutana ili kufanya ushirika, kula, na kusherehekea Meza ya Bwana, kusikia Maandiko yakisomwa na kuhubiriwa, kusali na kuimba nyimbo za sifa na shukrani kwa Mungu, na pia kuwabatiza waamini wapya na kuombea uponyaji. Matendo haya hayakuwa yamefungamanishwa na mahali popote (kwa maana ya eneo la kijiografia au jengo), na yalifanyika kwa msingi na mapekeo ya Kikristo. Neno “liturujia,” ni neno linalotumika kumaanisha kalenda au utaratibu wa huduma ambayo makusanyiko hutumia wanapoabudu pamoja.

2

1. Kanisa linapokusanyika, tunamwabudu Mungu kupitia mahubiri ya Neno la Mungu.

a. Liturujia, au ratiba na kalenda ya ibada, hufuata na kukariri matendo makuu ya Mungu katika historia.

b. Kanisa kupitia liturujia yake hukumbuka na kutafakari juu ya hadithi moja, ya kweli na kuu ya Mungu katika Maandiko.

c. Na tunapohubiri na kufundisha Neno la Mungu kama hadithi ya Mungu, tunaongozwa kumwabudu Mungu, kuelezea kustaajabishwa na kusherehekea kwetu yale ambayo Mungu ametenda kupitia watu wake na kupitia Yesu Kristo.

Made with FlippingBook flipbook maker