Theology of the Church, Swahili Student Workbook

/ 8 3

THEOLOJIA YA KANISA

ya makanisa yanaonekana kukua, yakiwa na wafanyakazi wengi, pesa nyingi, na shughuli nyingi, huku makanisa mengine, ambayo wakati mwingine yanaoneka kuwa ya kiroho zaidi, yanapambana ili yasifunge milango na kushindwa kuendelea. Baadhi ya huduma zinaonekana kupata kila aina ya umaarufu na rasilimali wakati hazionekani kuwa za kibiblia na zenye uaminifu kama zingine tunazojua, ambazo zinafanya kazi katika mazingira magumu ya kiuchumi. Baadhi ya wanafunzi walianza kukubaliana na mwelekeo huu wa fikra. Je, ungeitikiaje mjadala huu kuhusu Mungu na «upendeleo» wake?

Uchaguzi

Katika ulimwengu wetu, tunatumia neno «uchaguzi» kuelezea mchakato ambao tunachagua viongozi wetu wa kisiasa na «kuchaguliwa» kunamaanisha kuchaguliwa na wapiga kura kwa nafasi maalum ya uwajibikaji. Agano la Kale na Agano Jipya hutumia neno hili linapozungumza kuhusu watu wa Mungu kuwa “waliochaguliwa.” Je, Maandiko yanatumiaje neno “wateule” sawa au tofauti na matumizi yetu ya kisasa ya neno hili?

2

3

Ushuhuda

Hakuna hata mmoja wetu aliyezaliwa akiwa Mkristo. Tunapaswa “kuzaliwa mara ya pili” ili kuupokea Ufalme wa Mungu. Mungu alitumia nini kukushawishi kuwa Mkristo?

3

Kanisa kama Shahidi Sehemu ya 1

YALIYOMO

Mch. Dkt. Don L. Davis

Bwana Mungu, kama Mungu mkuu na mwenye mamlaka, amewaita na kuwachagua watu fulani kwa malengo na hadhi fulani. Zaidi ya yote, Mungu amemchagua Yesu wa Nazareti kuwa Mtumishi wake Mteule, Mwenye Kuteseka. Kupitia Yeye, Mungu amechagua kuleta wokovu kwa wanadamu wote, kwa kila mtu anayeshikamana naye kwa imani katika kifo chake, kuzikwa na kufufuka kwake. Mungu pia amewachagua Israeli kuwa chombo ambacho kupitia hicho angemleta Masihi ulimwenguni, na ambacho kupitia hicho atatupatia picha ya wazi ya wokovu wake uliotolewa kwa Wayahudi na mataifa katika Yesu Kristo. Waamini mmoja-mmoja wamechaguliwa “katika Kristo,” kupitia muungano na

Muhtasari wa Sehemu ya 1

Made with FlippingBook flipbook maker