Theology of the Church, Swahili Student Workbook

8 4 /

THEOLOJIA YA KANISA

ushirika wao pamoja naye. Uchaguzi wa Mungu unatokana na kusudi na neema yake kuu, aliyowapa watu duni na dhaifu wa ulimwengu ili mtu yeyote asijisifu mbele zake. Uchaguzi wa Mungu ni thabiti na umehakikishwa, kwa hiyo tunaweza kuwa na uhakika wa wokovu wetu katika Yesu Kristo. Lengo letu la sehemu hii ya kwanza ya Kanisa kama Shahidi ni kukuwezesha kuona kwamba: • Bwana Mungu, kama Mungu mkuu na mwenye mamlaka, amewaita na kuwachagua watu fulani kwa malengo na hadhi fulani. • Zaidi ya yote, Mungu amemchagua Yesu wa Nazareti kuwa Mtumishi wake Mteule, Anayeteseka. Katika Yeye, Mungu amechagua kuleta wokovu kwa wanadamu wote, kwa kila mtu anayeshikamana naye kwa imani katika kifo chake, kuzikwa na kufufuka kwake. • Mungu aliichagua Israeli kuwa chombo ambacho kwacho angemleta Masihi ulimwenguni, na ambacho kupitia hicho atatupatia picha ya wazi ya wokovu wake uliotolewa kwa Wayahudi na mataifa katika Yesu Kristo. • Waamini binafsi huchaguliwa “katika Kristo” kupitia muungano wao na ushirika pamoja naye. • Uchaguzi wa Mungu unategemea kusudi lake na neema yake kuu, iliyotolewa kwa wanyonge na dhaifu wa ulimwengu ili mtu yeyote asijisifu mbele zake. • Uchaguzi wa Mungu ni thabiti na umehakikishwa, kwa sababu hiyo tunaweza kuwa na uhakika wa wokovu wetu katika Yesu Kristo. I. Ili kuelewa kusudi la uchaguzi wa Mungu, ni lazima tukiri kwamba Yesu Kristo ndiye Mteule wa Mungu. Kati ya vipengele vyote vya fundisho la uchaguzi kama linavyohusiana na Kanisa katika ushuhuda wake, hakuna kipengele ambacho ni muhimu kama kile ambacho Biblia inasema kuhusu Yesu Kristo.

3

Muhtasari wa Sehemu ya 1 ya Video

A. Ndiyo, Yesu ana vyeo vinavyothibitisha kwamba yeye ni Mtumishi Mteule wa Mungu Mwenyezi.

Made with FlippingBook flipbook maker