Theology of the Church, Swahili Student Workbook

/ 8 5

THEOLOJIA YA KANISA

1. Yesu ndiye Mteule ( elektos ) wa Mungu, Mt. 16:16.

2. Yesu kama Jiwe la Thamani la Mungu, Jiwe la Pembeni la Jengo la Mungu; Yeye ni jiwe la Mungu, teule na la thamani, jiwe lililokataliwa na waashi, ambalo Mungu ameliweka kuwa jiwe kuu la Pembeni.

a. 1 Pet. 2:4

b. Zab. 118:22-23

3. Zaidi ya hayo, Yesu ni Mwana pekee na mpendwa wa Mungu, ambaye tunapaswa kumsikiliza na kumwamini.

3

a. Yoh. 1:34

b. Luka 9:35

c. Rej. Yoh. 6:35

4. Wale waliomdharau alipokuwa msalabani walimdhihaki kwa jina la “Kristo wa Mungu, mteule wake,” Lk. 23:35.

B. Yesu pia ni Mtumishi wa Yehova, aliyechaguliwa kumwakilisha katika kuufunua utukufu wake na kuukomboa ulimwengu.

1. Nyimbo za Mtumishi katika Isaya (rej. Isa. 41:8-9 na Isaya 42:1)

Made with FlippingBook flipbook maker