Theology of the Church, Swahili Student Workbook
/ 8 9
THEOLOJIA YA KANISA
a. Israeli inaundwa na tabaka mbili tofauti: (1) Wale wazao wasioamini wa Ibrahimu, (2) Mabaki ya wateule wanaoamini ambao wataepushwa na uharibifu kwa rehema ya Mungu. b. Hawa mabaki wateule wa Israeli (ambao ni wa nasaba yake ya kimwili) wanakuja kwa Mungu kupitia imani katika Kristo kwa njia ya Injili. (1) Rum. 11:1-2 (2) Rum. 11:7
c. Kulingana na Paulo, mabaki haya ndani ya Israeli wote ni “waliochaguliwa kwa neema” (Rum. 11:5) na walijulikana kabla (Rum.11:2).
3
d. Baada ya Mataifa kuingia katika wokovu, Paulo anasema kwa ujasiri kwamba “Israeli wote wataokolewa” (Warumi 11:26, nukuu ya Isaya 59:20-21). Kwa mujibu wa Paulo, Waisraeli watatunzwa na kuchaguliwa na Mungu kwa ajili ya baba yao mpendwa na hivyo watajumuishwa katika wateule wa mwisho wa Mungu (Rum. 11:28-29). B. Mungu pia amewachagua watu wake wateule – Kanisa kwa ajili wokovu, Wayahudi na mataifa, kwa njia ya imani katika kazi iliyokamilika ya Yesu msalabani. Mafundisho ya Maandiko yako wazi kwamba Mungu amewachagua Wayahudi na mataifa kuokolewa kwa njia ya imani katika Yesu Kristo.
1. Watu wa Mataifa wanaomwamini Yesu Kristo wamejumuishwa katika uchaguzi wa wokovu wa Mungu.
Made with FlippingBook flipbook maker