Theology of the Church, Swahili Student Workbook

9 4 /

THEOLOJIA YA KANISA

2. Katika kusudi la Mungu la kuchagua, anafunua wingi wa wema wake kwetu, upendo ambao tulipewa kabla ya kuwekwa misingi ya dunia, lakini sasa umefunuliwa kwetu katika Yesu Kristo.

C. Maana ya tatu ya uchaguzi wa Mungu ni kwamba uinjilisti na umisheni ni muhimu, pamoja na tumaini la hakika tulilo nalo katika neema ya Mungu ya kuchagua.

1. Ingawa Mungu Mwenyezi anawajua walio wake, sisi hatuwajui! Katika kutii Agizo Kuu, tunapaswa kutangaza Habari Njema hadi miisho kabisa ya dunia, tukifanya mataifa yote kuwa wanafunzi, tukiwafundisha kutii mafundisho ya Kristo (Mt. 28:18-20).

2. Mawazo matupu na yasiyofaa kwamba Mungu amekwisha kuamua ni kina nani waliopotea ambao yawapasa kuhukumiwa ni ukengeushaji wa kipumbavu dhidi ya mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa wazi ya kufanya wanafunzi hadi atakapokuja.

3

D. Maana ya nne na ya mwisho ni kwamba uchaguzi wa Mungu unampa Mungu uhakika kuhusu wale walio wake.

1. Mungu anawajua walio wake, 2 Tim. 2:15-19.

2. Hatupaswi kamwe kuhisi hatia kwa sababu ya wale wanaomkataa Yesu. Tunapaswa kumtangaza Yesu kama Bwana, na kuacha mengine kwa Roho wake kutenda.

3. Badala ya kubishana kuhusu masuala ambayo yanaweza kutatuliwa tu katika akili ya Mungu mwenyewe tunapaswa kukumbatia jukumu letu kama waamini, kuthibitisha fumbo la kusudi la Mungu la kuchagua, na mipaka ya ufahamu wetu. Huenda hatujui kamwe wale wote ambao tumewagusa, au sababu zilizo ndani ya moyo wa Mungu za uchaguzi wake mkuu. Tunaweza kuthibitisha, hata hivyo, kwamba

Made with FlippingBook flipbook maker