Theology of the Church, Swahili Student Workbook

/ 9 3

THEOLOJIA YA KANISA

c. Tunawasilisha habari njema ya wokovu kwa wote, tukijua kwamba wale wanaotubu na kuamini ni wateule wa Mungu, Mdo 13:48.

III. Hebu tufanye muhtasari wa sehemu hii muhimu kwa uchunguzi kadhaa kuhusiana na maana ya Uchaguzi wa Mungu.

A. Maana ya kwanza ni kwamba uchaguzi wa Mungu unaakisi utukufu wa ukuu na ubwana wake katika ulimwengu. Ikiwa Mungu ni Bwana katika mambo yote, hata kwa habari ya wokovu.

1. Bwana amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya (Mit. 16:4).

2. Kusudi kuu la Mungu kwetu litatimizwa, kwa hiyo wokovu wetu ni hakika na salama (Rum. 8:31-34).

3

3. Wakati hakuna yeyote aliyepatikana anayestahili kukitwaa kitabu kutoka kwake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, Mwana-Kondoo aliyeonekana kana kwamba amechinjwa alichukua heshima hiyo, na viumbe vya mbinguni vikatangaza kustahili kwake kukifungua kitabu hicho na kuzivunja mihuri zake (Ufu. 5:9-10).

4. Uteuzi wa Mungu kwa Kristo, Israeli, Kanisa, na watakatifu unadhihirisha chaguo lake kuu na tabia yake takatifu. Yeye ni Bwana peke yake.

B. Maana nyingine ya uchaguzi wa Mungu ni kwamba uchaguzi wake unaonyesha maajabu ya neema ya Mungu.

1. 2 Tim. 1:9-11

Made with FlippingBook flipbook maker