Theology of the Church, Swahili Student Workbook
9 2 /
THEOLOJIA YA KANISA
3. Tatu, Mungu alichagua watu wa hali ya chini, wanyonge na wapumbavu ili kuwaaibisha wenye hekima na wenye nguvu katika enzi hii, 1 Kor. 1:26-31.
4. Nne, hakuna mtu anayeweza kutilia shaka chaguo la Mungu la kumchagua Yesu, Israeli, au Kanisa. Uteuzi wa Mungu unabubujika kutoka katika kusudi lake kuu na chaguo lake mwenyewe, na haushawishwi wala kuamuliwa na hila za nje.
a. Hakika, katika mambo yote Mungu hutenda kulingana na mapenzi yake mwenyewe, Zab. 135:6.
b. Rum. 9:18-24
3
5. Tano, uchaguzi wa Mungu ni thabiti kabisa kwa habari ya wokovu wa wale anaowaita.
a. Rum. 8:38-39
b. Rum. 11:29
6. Na mwisho, maelezo ya wazi ya upotevu wa wanadamu yamewekwa sambamba na mialiko iliyo wazi na tayari ambayo Mungu anatupa sisi ili tuweze kuokolewa. Uchaguzi wa Mungu ni jambo la Mungu.
a. Yoh. 5:24
b. Yoh. 6:40
Made with FlippingBook flipbook maker