Theology of the Church, Swahili Student Workbook

/ 9 1

THEOLOJIA YA KANISA

g. Eze. 33:11

3. Mungu kibinafsi huchagua watu binafsi kwa ajili ya wokovu, akihakikisha milele ukombozi wao wa hakika na uliobarikiwa.

a. Mungu amehakikisha wokovu wa watu wake mwenyewe kupitia uwezo wake wa kujua mambo yajayo na uamuzi wake kwa habari ya maisha, Rum. 8:28-30.

b. Mungu amewachagua wale wanaomwamini Yesu Kristo kwa ajili ya wokovu, kuwa wanufaika wa uzima wake wa milele, Efe. 1:4-6.

c. Wote ambao Baba humpa Yesu watakuja kwake, Yoh. 6:37; na hakuna awezaye kuja kwa Kristo isipokuwa amevutwa na Baba, Yoh 6:44.

3

d. Alituchagua na kutuweka ili tuzae matunda yanayodumu (Yoh. 15:16).

C. Mjadala huu wa makusudi ya Mungu ya kuchagua unazaa kanuni kadha wa kadha.

1. Kwanza, rehema ya Mungu haitolewi kwa msingi wa jitihada na sifa za kibinadamu, bali kwa msingi wa fadhili na neema ya Mungu pekee; Kutoka 33:19 imenukuliwa katika Warumi 9:15-16.

2. Pili, uchaguzi wa Mungu unafanywa kwa msingi wa kusudi lake kuu kwa namna ambayo hakuna mtu anayeweza kujivunia haki au utakatifu wake mwenyewe, Efe. 2:8-9.

Made with FlippingBook flipbook maker