Theology of the Church, Swahili Student Workbook
9 6 /
THEOLOJIA YA KANISA
4. Ni katika njia zipi taifa la Israeli limetumikia kama ishara na mtangulizi wa watu wa Mungu wateule? Kulingana na Maandiko, ni baadhi ya sababu zipi za Mungu kuichagua Israeli kuwa taifa kupitia agano lake na Abrahamu? 5. Ni kwa njia gani leo tunaweza kusema kwamba Mungu pia amechagua Kanisa kuwa wakala na mwakilishi wake ulimwenguni? Je, kuna umuhimu gani kwamba Mungu amewachagua Wayahudi na mataifa kuwa washiriki wa Kanisa la Mungu katika Yesu Kristo? 6. Ni nini baadhi ya athari zinazotokana na ufahamu wa kibiblia wa uchaguzi wa Mungu kwa Yesu, Israeli, na Kanisa? 7. Ni kwa jinsi gani fundisho la kuchaguliwa linaweza kutilia mkazo kwetu uelewa wetu wa utukufu wa ukuu wa Mungu, ajabu ya neema yake, asili muhimu ya uinjilisti, na uhakika wa wokovu wetu? Toa majibu kwa kila kipengele hapa.
3
Kanisa kama Shahidi Sehemu ya 2
Mch. Dkt. Don L. Davis
Jukumu ambalo Yesu alitoa kwa Kanisa lake kuwa mashahidi wake limeelezwa kwa muhtasari katika Agizo Kuu. Utume huu unaweza kuelezewa kwa urahisi kulingana na vipengele vitatu muhimu, ambavyo vinaunda utume wa Kanisa ulimwenguni leo. Kipengele cha kwanza kinahusisha kazi ya “kwenda kuwafanya mataifa yote kuwa wanafunzi,” ambacho kinalielekeza Kanisa kutangaza Injilisha kwa waliopotea. Kisha, Kanisa linatoa ushahidi kwa “kuwabatiza katika jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu,” yaani, tumeitwa kubatiza waamini wapya katika Kristo tukiwajumuisha kama washirika katika Kanisa. Hatimaye, Kanisa linatoa ushahidi kupitia “kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi”; kwa maneno mengine, Kanisa la Yesu Kristo linafundisha washirika wake kutii mambo yote ambayo Kristo aliamuru. Mathayo 28:18-20 – Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. 19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho
Muhtasari wa Sehemu ya 2
Made with FlippingBook flipbook maker