Theology of the Church, Swahili Student Workbook

/ 9 7

THEOLOJIA YA KANISA

Mtakatifu; 20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. Amri hii ya kimungu inaangazia mwelekeo wa ushuhuda wa Kanisa kwa habari ya Kristo na Ufalme wake katika enzi hii ya sasa. Tutagawanya amri ya Kristo katika sehemu zake mbalimbali, na kwa ufupi tuangalie kila kipengele cha agizo la Yesu. Lengo letu la sehemu hii ya pili ya Kanisa kama Shahidi ni kukuwezesha kuona kwamba: • Jukumu ambalo Yesu alitoa kwa Kanisa lake kuwa mashahidi wake limeelezwa kwa muhtasari katika Agizo Kuu. • Utume huu unaweza kuelezewa kwa urahisi kulingana na vipengele vitatu muhimu, ambavyo vinaunda utume wa Kanisa ulimwenguni leo. • Kipengele cha kwanza ni kwamba Kanisa linatoa ushuhuda linapokwenda: Kanisa la Yesu Kristo limeitwa kutangaza Injili kwa waliopotea. • Kipengele cha pili ni kwamba Kanisa linatoa ushuhuda kwa njia ya ubatizo: Kanisa limeitwa kubatiza waamini wapya katika Kristo, yaani, kuwajumuisha kama washirika katika Kanisa. • Kipengele cha tatu ni kwamba Kanisa linatoa ushuhuda kupitia mafundisho yake: Kanisa la Yesu Kristo linafundisha washirika wake kushika mambo yote ambayo Kristo aliamuru, na hivyo kukua hadi kukomaa ndani yake.

3

I. Kipengele cha kwanza cha Agizo Kuu ni amri ya Yesu ya kwenda. Sisi kama Kanisa tunamshuhudia Yesu kwa kwenda ulimwenguni. Tunatoa ushahidi tunapoitikia wito wa kutangaza Injili.

Muhtasari wa Sehemu ya 2 ya Video

A. Wito wa kushuhudia ni wito wa kutangaza Habari Njema, wito wa kuinjilisha, kwenda ulimwenguni kote na kuhubiri Injili.

1. Hali ya kitenzi cha Kiyunani katika agizo la Yesu inatoa maana ya “kuendelea kwenda.” Kulingana na Yesu, Kanisa linapaswa “kuwa linaenda katika ulimwengu”; uinjilisti ni kazi ya Kanisa.

2. Tunapaswa kwenda ulimwenguni kote na kuhubiri Habari Njema kwa kila mtu (Mk. 16:15-16).

Made with FlippingBook flipbook maker