Theology of the Church, Swahili Student Workbook

9 8 /

THEOLOJIA YA KANISA

3. Katika Matendo 1:8, Kristo mwenyewe anaweka wazi mwelekeo wa kimataifa wa wito huu wa kushuhudia (yaani, Yerusalemu, Yudea, Samaria, na hata sehemu za miisho ya dunia).

4. Hili ni jukumu la kwenda katika kila taifa, kila jimbo, katika kila utamaduni na ukoo ili kutangaza waziwazi habari njema za Ufalme kwa wale ambao bado hawajasikia juu ya upendo wa Mungu katika Yesu Kristo (Rum. 15:20-21).

B. Wito wa uinjilisti unahusiana moja kwa moja na wajibu wa kuwa wahudumu wa upatanisho (2 Kor. 5:18-21).

1. Mungu alikuwa ndani ya Kristo akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake.

3

2. Mungu amelipatia Kanisa huduma ya upatanisho na sasa, kupitia sisi, anauita ulimwengu upatanishwe naye kwa njia ya Kristo.

3. Hatimaye, kama mabalozi wa Yesu Kristo, tunatoa ushahidi wa neema ya Mungu iokoayo katika Kristo katika ulimwengu, tukiwaalika wote kupokea rehema ya Mungu kupitia Mwanawe Yesu Kristo, na kuepuka hukumu yake.

C. Zaidi ya hayo, Agano Jipya linatuambia ni namna gani tunapaswa kwenda. Tunapoenda ulimwenguni kutangaza Injili, tunapaswa kuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote tupate kuwaokoa watu (1 Kor. 9:19-23).

1. Tunapaswa kuwasilisha kweli ya Injili kwa njia ambazo waliopotea wanaweza kuelewa, tukitumia uhuru wetu katika Kristo kufanya Habari Njema kuwa wazi na rahisi.

Made with FlippingBook flipbook maker