Theolojia Katika Picha
/ 1 2 1
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Kuchagua Vigezo vya Uhuru Vinavyoaminika (muendelezo)
d. Watumishi katika huduma ya kichungaji kuendelea kuwajenga washirika wa kanisa ili kuwawezesha kufanya kazi za huduma. e. Uratibu makini wa ibada, mafundisho, ushirika, na umisheni unaofadhiliwa na kuendeshwa na watenda kazi na washirika wa kanisa. 6. Kuzalisha Rasilimali na Mapato kwa ajili ya Huduma na Uendeshaji pasipo Msaada wa Wamishenari a. Imani thabiti na ya kina ndani ya kusanyiko kwamba watamtegemea Mungu pekee kuwa chanzo cha mahitaji yao kwa ajili ya kutekeleza maono ya kanisa lao. b. Kuweka mpango wa kulifanya kusanyiko kuwa huru kifedha na kutotegemea usaidizi wa wamishenari kutoka nje. c. Miongozo ya wazi ya namna ambayo uwezeshaji na misaada inaweza kutolewa kwa Mwili. d. Kubainisha vyanzo huru vya upatikanaji endelevu wa rasilimali fedha ambazo zitasaidia kufadhili shughuli za kanisa. 7. Upatikanaji na Uwakili wa Vyombo, Rasilimali, na Vifaa vya Kanisa a. Mifumo inayofanya kazi, rahisi kutumia iliyowekwa kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli na usimamizi wa kanisa. b. Orodha na hesabu makini na endelevu ya rasilimali za kanisa. c. Kuweka wazi kumbukumbu za hazina na fedha, manunuzi na ugavi wa kanisa. d. Uaminifu na umakini katika manunuzi na utunzaji wa vifaa na miundombinu ya kanisa. 8. Kujenga Marafiki, Ndugu, Watu wa Kujitolea, na Washirika Wenza Wapya a. Kutambuliwa na jumuiya nyingine za Kikristo ndani na nje ya jamii. b. Mahusiano mapya na makanisa ya nje au mashirika mengine ambayo yataendelea kuunga mkono juhudi kwa kutuma vikundi vya watenda kazi na usaidizi wa muda mfupi. c. Mahusiano mapya na madhehebu ya kanisa au vikundi ambavyo maono yao yanahusiana na kanisa. d. Ushirikiano wa kitaasisi kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa shughuli za kuifikia jamii na umisheni wa kanisa.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software