Theolojia Katika Picha

1 2 8 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Kuendeleza Ufalme Mjini (muendelezo)

Kushiriki Utambulisho, Kusudi na Dhamira ya Pamoja

Kuyachukulia makanisa kama yenye msingi wa uhusiano katika historia, utambulisho, urithi, na hatima.

Jina na Muungano wa Pamoja

Kukuza maono ya pamoja ya kitheolojia na kimafundisho

Ungamo la Pamoja la Imani

Maadhimisho na Ibada ya Pamoja

Kuwa na liturujia na mifumo ya kiibada ya pamoja

Kushiriki mtaala na utaratibu wa pamoja wa kukaribisha, kujumuisha, na kuwafuasa waamini wapya katika ushirika wetu.

Ufuasi na Katekisimu ya Pamoja

Utawala na Uangalizi wa Pamoja

Kuwajibika sehemu moja kwa ajili ya maongozi na huduma

Kukuza michakato na programu zilizounganishwa za kukuza haki, matendo mema, huduma za jamii, uinjilisti na umisheni, nyumbani na ulimwenguni kote.

Huduma na Umisheni wa Pamoja

Uwakili na Ushirikiano wa Pamoja

Kuunganisha rasilimali kupitia mchango thabiti wa pande zote ili kuongeza ufanisi wa jumuiya nzima.

Faida za Jumuiya ya Pamoja

1. Hisia ya kuhusishwa kupitia imani na utambulisho wa pamoja. 2. Ufanisi na iktisadi ya juhudi za jumuiya.

3. Uwezo wa kupanda makanisa mengi katika maeneo mengi na jamii tofauti za watu. 4. K ukuza umoja na utofauti wa kweli, kwa moyo wa kuheshimiana na usawa miongoni mwa makusanyiko. 5. Kuongezeka kwa tija na ufanisi ndani ya makanisa na juhudi zetu za kimisheni. 6. Kubadilishana uzoefu na kuwezeshana. 7. Kuwaunga mkono na ukuwatia moyo viongozi wetu kwa namna endelevu. 8. Kuwezesha utekelezaji wa miradi mipya na mipango mipya. 9. Michakato na taratibu sanifu za ujumuishaji na mafunzo. 10. F ursa kubwa zaidi za kukutana na kukaa pamoja na waamini wengine wenye nia moja nasi.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software