Theolojia Katika Picha
/ 1 2 7
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Kuendeleza Ufalme Mjini Kuzidisha Makusanyiko Yenye Utambulisho wa Pamoja Mch. Dkt. Don L. Davis
Mdo 2:41-47 – Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. 42 Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali. 43 Kila mtu akaingiwa na hofu; ajabu nyingi na ishara zikafanywa na mitume. 44 Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika, 45 wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haja. 46 Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe, 47 wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa. Kanuni ya Utatu: Umoja • Utofauti • Usawa World Impact inalenga kupanda makanisa ambayo ni jumuiya zenye mtazamo wa Ufalme ambapo Kristo anainuliwa kama Bwana na Ufalme wa Mungu unakuzwa katika kila nyanja ya maisha ya jumuiya, na, tunatafuta kufanya hivi kwa njia ambayo inaheshimu na kukubali uhalali na umuhimu wa kuakisi maisha haya ya jumuiya katika utamaduni na jamii husika. Ili kuhakikisha uhai, ulinzi, na ustawi wa makusanyiko haya, tunapaswa kuzingatia kuunda ushirikiano wa karibu kati ya makusanyiko kwa namna ambayo inaleta umoja katika utambulisho, maungamo, na imani, chini ya uangalizi na utawala wa pamoja unaounganisha pamoja rasilimali na maono ya kila kanisa pasipo kuwatawala kiimla. Ifuatayo ni chati inayoonyesha vipengele vya muungano huo wa pamoja wa makanisa ambao unaweza kuunganisha maisha yao kwa njia ya kimkakati kwa ajili ya ustawi na utajiri wa ushirika mzima wa makanisa. (Taz. Kufikiria Harakati Zilizounganishwa za Kupanda Makanisa ya C1 [ona www.tumi.org/Capstone chini ya kichwa cha Viambatisho ] andiko ambalo kwa njia ya kina linapendekeza kile kinachoweza kujumuishwa katika miktadha ya kikanisa na kimishenari, liturujia, na katekesi katika ushirika kama huo). koinonia (matamshi: [koy-nohn-ee’-ah])
Made with FlippingBook Digital Publishing Software