Theolojia Katika Picha

1 2 6 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Kuelewa Maono ya Mungu kwa Watu Wake "Mshikamano wa Kudumu" katika Utafutaji Wetu wa Nchi ya Ahadi

Waebrania 11:13-16 – Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi. 14 Maana hao wasemao maneno kama hayo waonyesha wazi kwamba wanatafuta nchi yao wenyewe. 15 Na kama wangaliikumbuka nchi ile waliyotoka, wangalipata nafasi ya kurejea. 16 Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji. Kuna idadi kubwa ya taswira saidizi zinazohusiana na lugha ya picha ya "watu wa Mungu" kwa Wakristo na Kanisa la Kikristo. Hizo zinahusisha majina yafuatayo katika nyaraka za Paulo: “Wateule wa Mungu” ( Rum. 8:33; Efe. 1:4; Kol. 3:12 ), “wazao wa Ibrahamu” (Rum. 4:16; Gal. 3:29; 4:26-28), “Tohara ya kweli” ( Flp. 3:3; Kol. 2:11 ), na hata “Israeli wa Mungu” ( Gal. 6:16 ). Picha hizi zote zinasisitiza, kwa namna fulani, mshikamano wa kudumu wa watu wa Kanisa na watu wa Israeli, ambao historia yao inalipa kanisa ushuhuda wenye mamlaka wa kanuni na matendo yanayohusiana na kazi ya ukombozi ya Mungu katika zama za kale. Ni kazi ya eksejesia na theolojia kubainisha asili ya uhusiano huu. ~ Richard Longenecker, ed. Community Formation in the Early Church and in the Church Today. Peabody, MA: Hendrickson Publishers, 2002. uk. 75.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software