Theolojia Katika Picha

1 4 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Baraka Thelathini na Tatu Katika Kristo Mch. Dkt. Don L. Davis

Je, ulijua kuwa vitu thelathini na vitatu vilitokea kwako wakati ulipokuwa muumini katika Yesu Kristo? Lewis Sperry Chafer, Rais wa kwanza wa Seminari ya Kithiologia ya Dallas, aliorodhesha manufaa haya ya wokovu katika, Theology, volume 3 (pp. 234-266). Hoja hizi, pamoja na maelezo mafupi, yanampa Mkristo aliyezaliwa upya uelewa bora juu ya kazi ya neema iliyotimizwa katika maisha yake pamoja na shukrani ya maisha yake mapya. 1. Katika mpango wa milele wa Mungu mwumini ni a. Alimjua tangu asili – Matendo 2.23; 1Pet. 1.2, 20. Mungu alimjua tangu milele yote kila hatua katika utaratibu wote wa ulimwengu. b. Aliwachagua tangu asili – Rum 8.29-30. Majaliwa ya mwumini yaliwekwa kwa kumjua tangu asili kwa utambuzi usio na mwisho wa utajiri wa neema ya Mungu. c. Aliteuliwa – Rum 8:38; Kol 3:12. Yeye ni mteule wa Mungu kwa wakati huu na atadhihirishwa wazi neema ya Mungu kwa wakati unaokuja. d. Kachaguliwa – Efe. 1.4. Mungu amewatenga kwake mwenyewe wateule wake ambao kwanza aliwajua tangu asili na kisha akawachagua. e. Kaitwa – 1 The. 5.24. Mungu anamwalika mtu kufurahia mafao ya makusudi ya kukombolewa kwake, sharti hili linaweza kuwaingiza wale ambao Mungu amewateua kwa ajili ya wokovu, ambao bado wamo katika hali ya kutozaliwa upya. 2. Waumini wamekombolewa – Rum 3.24. Bei iliyo hitajika kwa kumweka huru kutoka katika dhambi imekwisha lipwa. 3. Muumini amekwisha patanishwa – 2 Kor. 6.18; Rum. 5.10. Kwanza amekwisha kurejeshwa na Mungu kwenye ushirika kisha karejeshwa kuwa na ushirika na Mungu. 4. M wumini anahusiana na Mungu kwa njia ya upatanisho – Rum. 3.24-26. Amewekwa huru kutoka kwenye hukumu kwa ridhaa ya Mungu kwa kifo cha mwanae kwa ajili ya wenye dhambi. 5. Mwumini amesamehewa makosa yote – Efe. 1.7. Dhambi zake zote zinashughulikiwa –zilizopita, za sasa, na zijazo. 6. M uumini kwa ulazima wa uzima ameungwa kwa Kristo kwa hukumu ya mtu wa kale na kuwa katika “mwenendo mpya” - Warumi 6:1-10. Mwamini ameingizwa katika mwungano na Kristo.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software