Theolojia Katika Picha

/ 1 5

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Baraka Thelathini na Tatu Katika Kristo (muendelezo)

7. M wumini ni huru “kutoka sheria” - Rum 7.2-6. Ameifia hukumu yake na kufunguliwa kutoka katika mamlaka yake ya kisheria. 8. Mwumini amefanyika mtoto wa Mungu - Gal 3.26. Amezaliwa upya kwa uwezo wa Roho Mtakatifu wa kumleta kwa upya katika uhusiano ambao Mungu nafsi ya kwanza anakuwa Baba halali na, aliyeokolewa anafanyika kuwa mototo halali kwa kila haki na cheo –mrithi wa Mungu na mrithi pamoja na Yesu Kristo. 9. M wumini amefanyika mototo wa kulelewa akiwa mtu mzima nyumbani mwa Baba yake – Rum.8.15, 23 10. M wumini amefanywa na Yesu Kristo akubalike na Mungu na Yesu Kristo – Efe. 1.6. Amehesabiwa haki (Rum.3.22), ametakaswa (ametengwa) nafsi (1Kor.1.30, 6.11); amekamilishwa hata milele katika msimamo na nafsi yake (Ebr 10.14), na kufanywa kukubalika katika mwanae mpendwa (Kol 1.12) 11. Mwumini amehesabiwa haki – Rum.5.1. Ametangaziwa kuwa mwenye haki kwa amri ya Mungu. 12. M wumini anafanywa mwenye haki – Efe.2.13. Uhusiano wa karibu unaanzishwa na unakuwapo kati ya Mungu na mwumini Uhusiano wa karibu umewekwa na ipo kati ya Mungu na muumini. 13. Mwumini amefunguliwa kutoka katika nguvu za giza – Kol.1.13; 2.13. Mkristo amefunguliwa kutoka kwa shetani na roho zake chafu. Hata hivyo mwanafunzi anatakiwa kupigana vita dhidi ya nguvu hizi. 14. Mwumini amehamishiwa katika ufalme wa Mungu - Kol 1:13. Mkristo amehamishwa kutoka katika ufaalme wa giza kwenda ufalme wa Kristo. 15. Mwumini amepandwa katika mwamba, Yesu Kristo - 1Wakor 3:9-15 Kristo ni msingi ambao mwumini anasimama na ambapo anajenga maisha yake ya Kristo. 16. Mwumini ni zawadi kutokakwaMungukwendakwaKristo -Yoh.17:6,11,12,20. Yeye ni zawadi ya upendo wa Baba kwa Yesu Kristo. 17. Mwumini ametahiriwa katika Kristo - Wakol. 2:11. Ameokolewa kutoka nguvu za asili ya dhambi ya kale. 18. Mwumini amefanywa kuwa mshiriki wa ukuhani mtakatifu na ukuhani wa Kifalme - 1Pet2:5,9 Yeye ni kuhani kwasababu ya uhusiano wake kwa Kristo, kuhani mkuu, na atatawala duniani na Kristo. 19. M wumini ni sehemu ya kizazi kiteule, taifa takatifu watu wa ajabu -1Pet.2:9 Hili ni jeshi la waumini katika zamani hizi.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software