Theolojia Katika Picha
1 6 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Baraka Thelathini na Tatu Katika Kristo (muendelezo)
20. Mwumini ni raia wa mbinguni – Flp 3.20. Kwa hiyo anaitwa mgeni kama yalivyo maisha yake hapa duniani (1Pet.2:13) na atafurahia maisha yake ya nyumbani ya kweli huko mbinguni milele. 21. Mwumini yuko katika familia ya Mungu na nyumbani mwake. – Efe. 2.1, 9. Yeye ni sehemu ya “Familia” ya Mungu ambayo inaundwa pekee na waumini wa kweli. 22. Mwumini yumo katika ushirika wa watakatifu – Yohana 17.11, 21-23. Yeye anaweza kuwa sehemu ya ushirika wa waumini moja kwa mwingine. 23. M wumini yumo katika Ushirika wa mbinguni – Kol. 1.27; 3.1; 2 Kor 6.1; Kol. 1.24; Yohana 14.12-14; Efe. 5.25-27; Tit 2.13. Yeye ni mshirika na Kristo sasa katika maisha, mahali, huduma, mateso sala, uposo kama bibi arusi wa Kristo na matarajio ya kuja tena kwa Kristo. 24. Mwumini ana nafasi ya kumfikia Mungu – Efe 2.18. Yeye ana njia ya kupata neema ya Mungu ambayo inamwezesha kukua kiroho na hana kizuizi cha kumkaribia Baba (Waeb.4:16) 25. Mwumini yuko katika uangalizi sana wa Mungu – Rum. 5.8-10. Yeye ni mlengwa wa pendo la Mungu (Yoh.3:16) neema ya Mungu (Waef.2:7,9), nguvu za Mungu (Waef 1:19), uaminifu wa Mungu (Wafil.1:6), Amani ya Mungu (Warumi 5:10 faraja ya Mungu (2 Wathes.2:16-17), na maombezi ya Mungu (Warumi 8:26). 26. Mwumini ni urithi wa Mungu – Efe 1.18 yeye ametolewa kwa Kristo kama zawadi kutoka kwa mungu 27. Mwumini anao urithi wa Mungu mwenyewe uliotunzwa - 1Petro 1:4 28. Mwumini ana nuru katika Bwana – 2 Kor. 4.6 si kwamba tu anayo. Hii nuru, bali ameagizwa kutembea nuruni 29. M wumini kwa umuhimu ameungana na Baba na mwana na Roho Mtakatifu – 1The 1.1; Efe 4.6; Rum 8.1; Yohana 14.20; Rum.8.9; 1Kor. 2.12. 30. M wumini amebarikiwa na matunda ya kwanza ya Roho – Efe. 1.14; 8.23. Amezaliwa kwa Roho (Yoh.3:6) na kubatizwa kwa Roho (1Wakor.12:13) ambayo ni kazi ya Roho Mtakatifu ambayo kwayo mwumini huunganishwa kwa mwili w kristo na anakuja kuwa “ndani ya Kristo” na kwa hiyo anakuwa mshirika wa yote Kristo alivyo. Mwanafunzi pia anakuwa na Roho Matakatifu anaye kaa ndani yake (Warumi 8:9), ametiwa muhuri na Roho (2Kor.1:22) na kumfanya kuwa salama milele, na amejazwa na Roho (Waefeso 5:18) ambaye huduma yake ni kuachilia nguvu zake zinazofaa katika moyo anamokaa.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software