Theolojia Katika Picha

1 4 4 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Kushika Imani, Sio Dini (muendelezo)

dhaifu kwa habari Roho Mtakatifu na nguvu za kiroho, umejikita zaidi katika aina za mawasiliano (k.m. kuhubiri) na mifumo ya ibada ya kimagharibi na kulazimishwa kwa watu wasio wa Kimagharibi kana kwamba huo ndiyo Ukristo wa kibiblia. Mara nyingi ni rahisi kuchukulia kwamba muundo fulani wa muonekano wa Ukristo ni wa usawazishaji hasa wakati unapoakisi zaidi utamaduni pokezi kuliko unapoonekana wa “kawaida”, yaani, wa kimagharibi. Lakini mifumo ya Magharibi mara nyingi iko mbali zaidi na Biblia kuliko mifumo isiyo ya Magharibi. Na kiasi cha upotoshaji wa maana halisi ya Injili kinaeza kuwa kikubwa pale watu wanapodhani kwamba Ukristo ni dini badala ya imani na kwamba, kwa sababu hiyo, mifumo ya kigeni ni ya lazima. Kutoa hisia kama hiyo hakika ni kufanya usawazishaji na ni upotoshaji. Hiki ndicho kwa kawaida ninakiita “uzushi wa kimawasiliano.” Lakini, vipi kuusu dhana ya usawazishaji? Je, hili ni jambo linaloweza kuepukwa au ni jambo linalotokana na mipaka ya kibinadamu na dhambi? Kura yangu mimi ni kwa hili la mwisho na ninadhani kwamba hakuna namna ya kuliepuka. Popote palipo na uelewa usio kamili uliosababishwa na watu wasio wakamilifu, kutakuwa na usawazishaji wa imani. Kwamba usawazishaji upo katika makanisa yote sio tatizo. Kuwasaidia watu kuhama kutoka mahali walipo hadi kufikia namna bora ya kuielezea Imani ya Kikristo ndilo tunalohitaji kulishughulikia. Hata hivyo, maadam tunaogopa kitu ambacho hakiepukiki, tukokatika utumwa. Nakumbuka maneno ya mmishenari mmoja aliyekuwa akisoma nasi, “Mpaka nilipoacha kuwa na hofu kuhusu usawazashaji, sikuweza kufikiria ipasavyo kuhusu kuzingatia muktadha.” Hivyo basi, ushauri wetu kwa viongozi wa kitaifa (na kwa wamishenari) ni kuacha kuogopa usawazishaji. Ushughulikieni kwa namna mbalimbali kama sehemu ya kuanzia, kwamba umetokana na jamii pokezi au ni kutoka kwa jamii chanzi na uwasaidie watu kuelekea kwenye namna bora zaidi ya kuakisi imani yao … Kwa karne nyingi, wale ambao wamemjia Kristo wameelekea “kuufuga” Ukristo wao. Kama vile Wakristo wa kale wa Kiyahudi waliokuwa wakimpinga Paulo walivyowataka watu wa mataifa mengine kumkubali Kristo katika msingi wa utamaduni wa Kiyahudi, vivyo hivyo Warumi na Wajerumani na Wamarekani wamewashinikiza wale wanaomgeukia Kristo pia kuzigeukia tamaduni za wale wanaowaletea ujumbe. Hivyo basi, imani yetu imekuja kujulikana kimsingi kama kitu cha kitamaduni, dini iliyofungashwa katika miundo na mifumo ya kitamaduni ya kundi lililo na nguvu. Na kuanzia karne ya nne hivi na kuendelea imekuwa ikionekana kwa kiasi kikubwa kama Wenyeji na “Ukristo wa Kitamaduni”

Made with FlippingBook Digital Publishing Software