Theolojia Katika Picha

/ 1 4 5

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Kushika Imani, Sio Dini (muendelezo)

kitu cha utamaduni wa Ulaya – kilichokamatwa na mababu zetu wa Ulaya na kuingizwa kwenye utamaduni tofauti kabisa na le ambayo imani ilipandwa hapo kwanza. Wale wanaoongoka kuingia katika Ukristo, basi wanaonekana kama watu walioacha dini zao za kitamaduni na kuchagua kufuata dini na, kwa kawaida, mifumo mingi ya utamaduni wa Ulaya. Mara nyingi waongofu kama hao huchukuliwa kuwa wasaliti dhidi ya watu wao na njia zao. Ikiwa imani yetu ni “ni dini ya miundo na mifumo” tu, inaweza kuigwa lakini sio kuingizwa kwenye muktadha wa watu na jamii fulani , inaweza kuwa kwenye ushindani na miundo mingine ya dini lakini haiwezi kuakisiwa kupitia miundo hiyo kwa sababu kimsingi inatafuta kuchukua nafasi ya miundo hiyo. Lakini Ukristo wa Kibiblia sio mkusanyiko wa miundo ya kitamaduni. Japo Ukristo wa kitamaduni uko hivyo. Na tunachanganykiwa katika mijadala yetu kwa sababu mara nyingi haijulikani wazi kama tunazungumzia Ukristo halisi wa kibiblia au wa dini ya jadi ya jamii za Magharibi ambayo pia huitwa Ukristo. Katika mojawapo ya vitabu vyangu (1979a) nimejaribu kutofautisha kwa kuandika Ukristo wa kibiblia kwa herufi kubwa “U” na ukristo wa kitamaduni kwa herufi ndogo “u”…. Binafsi…. ningeita dini kuwa kitu cha kimuundo, kielelezo kupitia miundo ya kina ya kitamaduni ya dhana na maana (mtazamo). Miundo ya kidini ni mahususi kwa utamaduni na, ikiwa dini imekopwa kutoka kwa muktadha mwingine wa kitamaduni, inahitaji aina fulani za utamaduni huo mwingine kukopwa pia. Uislamu, kwa mfano, unahitaji namna fulani za maombi, hija, kitabu cha Kiarabu kisichoweza kutafsiriwa, hata mitindo ya mavazi. Kadhalika Uyahudi, Uhindu, Ubudha na Ukristo wa kitamaduni. Hizi ni dini. Ukristo halisi wa kibiblia, hata hivyo, hauhitaji muundo wowote wa asili wa kitamaduni. Hiyo ndiyo sababu unavyoweza “kukamatwa” na watu wa Magharibi na kuchukuliwa kama ni wa Kimagharibi ingawa asili yake si Magharibi. Ukristo halisi ni utii, uhusiano, ambao kupitia huo hutiririka mfululizo wa maana zilizokusudiwa kuakisiwa kupitia miundo ya utamaduni wowote. Hivyo basi, miundo hii imekusudiwa kuchaguliwa kwa kufaa kwake ili kuwasilisha maana sahihi za kibiblia katika muktadha wa wapokeaji. Ninaamini Ukristo umekusudiwa kuwa “imani,” sio mkusanyiko wa miundo ya kitamaduni, na kwa hiyo unatofautiana na dini hizo. Dini, kwa sababu ni mambo ya kitamaduni, zinaweza kurithishwa kwa tamaduni mpya. Urithishaji huo ni jambo la nje linalosababisha mabadiliko madogo au makubwa katika mifumo ya dini. Ukristo, hata hivyo, unaweza kuwekwa katika muktadha, mchakato ambao maana zifaazo zinaweza kubebwa katika muundo na mfumo tofauti kabisa ndani ya tamaduni mbalimbali. Kwa bahati mbaya, kwa sababu ya kuingiliwa kwa ukristo wa kitamaduni, hatujaona aina zote za utofauti zinazowezekana…

Made with FlippingBook Digital Publishing Software