Theolojia Katika Picha

1 5 4 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Kutafuta kwa Msafiri Don L. Davis

Kukaa kama wasafiri watafutao Mfalme Mkuu kumuona Ili kushiriki msingi mmoja, tumaini moja, ndoto moja

Kutembea bega kwa bega, kila mzigo tunaobeba Kwa imani yenye subira, kwa ukunjufu na uangalifu mkubwa

Katika urafiki na Kristo, Utukufu wetu na Taji yetu Kwamba ndani yake pekee, ipatikane ya kweli furaha yetu

Kuona kwa macho mapya thamani ya kila nafsi moja Kuithamini iliyo ndogo zaidi, kuliko vyote vya dunia

Kuwaka kwa shauku kubwa ili sifa zake zitiririke Na kwa umoja wetu mzuri, uonekane uzuri wake

Ndiyo, hili ndilo lengo letu, utukufu wetu, kusudi letu Ili Kristo aonekane tena hapa duniani Kwamba ujulikane sana, Ufalme wake na utukufu Ili mfano wake udhihirike zaidi kupitia sisi Kwamba kwa ajili ya marafiki zetu tuyatoe maisha yetu Ili matunda yake yazaliwe, na neema yake izidi

Kwamba kwa kushirikiana pamoja ziangaze sana taa zetu Ili ulimwengu uvutwe kwake, roho moja na moja zaidi Na kila chombo kilichovunjika, kiwe kipole na kinyenyekevu Tuonje rehema za Mola wetu, tuponywe, tuwekwe huru na Mwenyezi. Tunahesabu sasa kama mavi starehe zote tamu za ulimwengu huu Tunasonga mbele kuelekea lengo la kupata hazina za kweli za Ufalme Tunakualika ujiunge nasi katika azma yetu yenye utukufu Kusafiri nasi kwa furaha kama mgeni, kushuhudia kutawazwa kwake, Tunatoa vyote tulivyo na tulivyo navyo kwa jambo moja Kula hivi karibuni kwenye karamu yake mbele ya Kristo Mfalme Mkuu.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software