Theolojia Katika Picha
1 6 8 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Kuwa Mwangalifu kuhusu Picha Unayoakisi
Picha zina nguvu. Zinatengeneza kile tunachokiona, kwa kuangazia vipengele fulani na kusogeza vingine nyuma. Zinatawala mifumo yetu ya uchambuzi na tafakari. Zinatoa maelezo ya kwa nini tunahusiana jinsi tunavyohusiana, au kwa nini miundo fulani ipo. Zinategemeza uelewa fulani wa siku za nyuma, tafsiri za sasa, na hali za siku zijazo. Zinakuza maadili fulani na kupinga mengine. Zinapendekeza vipaumbele, na kuamsha hisia. Chaguo la kusisitiza sitiari fulani na kuweka kando nyingine linaweza kutoa mwelekeo wa jamii na uongozi wake . Kwa hiyo, ni lazima tuzifahamu picha tunazotumia, na jinsi tunavyozitumia. Hasa, lazima tuchunguze mafumbo na mifano tunayotumia katika kuwafundisha viongozi wetu wa baadaye . ~ David Bennett. Metaphors of Ministry. uk. 199.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software