Theolojia Katika Picha

1 7 0 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Kuwawezesha Watu kwa ajil ya Uhuru, Ustawi na Haki Misingi ya Kitheolojia na Kimaadili ya Huduma za Kimaendeleo za World Impact

Don Davis na Terry Cornett

Theolojia ya Maendeleo

Upendo kwa Mungu na upendo kwa jirani zimekuwa mada muhimu za theolojia ya Agano la Kale na Agano Jipya tangu mwanzo. Tangu wakati wa Kanisa la kwanza na kuendelea, kumekuwa na jitihada za kuonyesha upendo na tabia ya Mungu kwa ulimwengu kwa maneno na vitendo, kwa njia ya imani na matendo, kupitia kuhubiri Injili na matendo ya haki na wema. Kuanzia na watangulizi wake katika harakati za mageuzi na uamsho wa Puritan, Pietistic, Moravian, na Wesleyan, na kuendelea hadi kwenye harakati za kisasa za umishenari za Kiprotestanti, wamishenari wa kiinjili wameunganisha msisitizo mkubwa wa uinjilisti na uanzishwaji wa makanisa na jaribio la dhati la kujihusisha katika shughuli ambazo zinalenga kukuza haki na uadilifu, hasa kwa niaba ya watu maskini na walioonewa. Wanamageuzi na wamishenari wa Kiinjili wameanzisha shule na hospitali zenye lengo la kuhudumia watu wa hali ya chini zaidi katika jamii, wameanzisha vituo vya watoto yatima na kufanya kazi kushawishi marekebisho ya sheria za ajira ya watoto, kuanzisha biashara na ubia miongoni mwa watu maskini, kuunga mkono sheria ya kukomesha utumwa na kuhakikisha ulinzi wa haki za binadamu, walifanya kazi ya kuinua hadhi ya wanawake katika jamii, na kusuluhisha migogoro kati ya makundi na mataifa yanayopigana. 1 Ingawa Wakristo kwa ujumla wanakubali kwamba uinjilisti na huduma za kijamii ni wajibu muhimu wa Kanisa, kuna tofauti kubwa katika maneno yote mawili ambayo hutumiwa kumaanisha majukumu haya, na jinsi yanavyofafanuliwa na kuhusianishwa. Kama taasisi ya kimisheni ambayo inajishughulisha na shughuli hizi zote mbili, ni muhimu kujenga ufafanuzi wetu wa maneno haya na msimamo kuhusu uhusiano wa kitheolojia uliopo kati ya kazi hizi mbili.

Dibaji

1 Tazama makala ya Paul E. Pierson, “Missions and Community Development: A Historical Perspective,” (Elliston 1989, 1-22) umisheni wa Kiinjili na kitabu cha Donald W. Dayton “Discovering an Evangelical Heritage” (Dayton, 1988) kupata maarifa kuhusu harakati za mageuzi ya Kiinjili. kwa utangulizi wa historia ya kazi ya maendeleo katika

Made with FlippingBook Digital Publishing Software