Theolojia Katika Picha
/ 1 9 7
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)
Roho Mtakatifu atayaunganisha mambo hayo mawili kwa pamoja. Lakini makanisa yanayotegemea mashirika ya hisani karibu kila mara yanatawaliwa na wamishenari wa kigeni na ni nadra sana kuweza kuzaa makanisa mengine (Patterson 1992, D-80). Mara nyingi sana wachungaji na makanisa wenyeji wamejishughulisha na huduma zinazovutia dola za Magharibi (kama vile kuhudumia yatima) huku wakipuuza utunzaji wa msingi zaidi wa kichungaji na uinjilisti. Hata kazi ya maendeleo, isiposimamiwa kwa busara, inaweza kuzuia ukuaji wa kanisa (Ott 1993, 289). Kuna hatari kubwa sana ya kuajiri wamishenari-wainjilisti hasa kwa msingi wa uwezo na ujuzi wao. “Chochote ambacho ni taaluma yako, tunaweza kukitumia katika umisheni wetu” - hii ni njia ya kawaida sana ya kuajiri. Kwa hiyo, wafanyakazi wengi hufadhaika wakati ambapo taaluma zao na uwezo wao maalum hautumiki kikamilifu; wanaitikia kwa “kufanya mambo yao” tu na kuchangia kwa njia isiyo ya moja kwa moja tu kwa kazi ya upandaji makanisa yanayokua. Kwa hiyo, zile zinazoitwa huduma za ziada au wezeshi kuna namna zikuwa kama ndizo za msingi na kwa kweli hata kuweza kufunika kazi kuu! (Hesselgrave 1980, 112). Inasikitisha kwamba huduma za jamii na Injili mara nyingi huonekana kama dhana kinzani katika kazi ya uenezaji wa Imani ya kikristo wakati, kusema kweli, yote mawili ni ya kibiblia na yanakamilishana. . . . Sababu moja ya mvutano huu ni kwamba mashirika ya kikristo ya huduma za jamii kama vile hospitali na taasisi za elimu kuna namna yanaonekana kuchukua fedha na rasilimali nyingi na kuacha uinjilisti ukizongwa na mahitaji mengi (Hesselgrave 1980 p. 328). Kwa kuwa tunaamini katika umoja wa Biblia, ni lazima tuseme kwamba ‘Agizo Kuu si amri iliyojitenga, (bali) ni matokeo ya asili ya tabia ya Mungu... Kusudi la kimishenari na msukumo wa Mungu...’ Hivyo, tusichukue Amri Kuu na Agizo Kuu kana kwamba ni mambo yasiyo changamana. Tunapaswa kuchukua Amri Kuu—kuwapenda wengine— na Agizo Kuu—kuhubiri—pamoja, kwa kuyaunganisha katika umisheni wa Yesu Kristo, kwani ni Bwana yule yule, ambaye aliwaamuru na kuwaagiza wanafunzi na wafuasi wake wale wale. Kwa hivyo, kama Di Gangi asemavyo, ‘ili kueneza Injili kwa ufanisi ni lazima tutii Amri Kuu pamoja na Agizo Kuu’ (Cho 1985, 229).
Made with FlippingBook Digital Publishing Software