Theolojia Katika Picha
1 9 6 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)
• Vipengele hivi vya utendeaji kazi vinapaswa kufundishwa na kukaguliwa mara kwa mara. • Vipengele hivi vya utendeaji kazi vinapaswa kujumuishwa katika kila tathmini iliyoratibiwa inayofanywa mara kwa mara na mradi. • Kufuatia kila tathmini iliyoratibiwa, kunapaswa kuwa na marekebisho na kusasishwa kwa programu hizi kulingana na kile ambacho wahusika wamejifunza kupitia uzoefu.
Kiambatisho A
Nukuu Zilizochaguliwa kuhusu Jukumu la Kazi ya Maendeleo ndani ya Taasisi ya Kimisheni
Mabadiliko ya kijamii katika msingi wa Kikristo yanatofautiana na unafuu na maendeleo ya kidunia kwa kuwa yanatumika katika uhusiano uliojumuishwa, wa ulinganifu na huduma zingine za Kanisa, ikijumuisha uinjilisti na upandaji makanisa (Elliston 1989, 172). Uzoefu wangu wa huduma nyingi miongoni mwa jamii maskini umenifundisha kwamba miradi ya kiuchumi, inapotumiwa kama mbinu za kuingia katika jamii hizo, haifanikishi upandaji na ukuzaji wa makanisa. . . . malengo haya mawili—misaada na upandaji makanisa—ni malengo tofauti. Yote mawili ni ya Kikristo, na wakati fulani wanaenda pamoja. Lakini mara nyingi hayasaidiani vizuri hata kidogo. . . . Inaonekana kwamba pale watenda kazi wanapoingia katika jamii wakiwa na kipaumbele cha kutangaza Injili, kunakuwa na matendo mengi ya huruma (kusaidia wahitaji), matendo ya haki na ishara vikiambatana na kazi ya Injili. Kutokana na haya makanisa yanaanzishwa. Lakini watenda kazi wanapoingia wakiwa na kipaumbele cha kushughulikia mahitaji ya kiuchumi, wanaweza kuwasaidia watu kiuchumi vizuri sana, lakini ni mara chache sana wanaanzisha kanisa. Kuna wakati kwa ajili yote mawili, na kuna waliopokea wito wa maisha wa kufanya yote mawili, lakini ni lazima yatofautishwe (Grigg 1992, 163-64). Epukana na taasisi kama inawezekana katika hatua za awali (mipango ya maendeleo ya jamii isiyohusiana na upandaji makanisa, shule, zahanati, n.k.); hayo yatakuja baadae. Huko Honduras tulibuni kazi za maendeleo ya jamii lakini zilikuja kupitia makanisa, sio kinyume chake. Tulifundisha watu utii kwa amri kuu ya kumpenda jirani yetu kwa njia ya vitendo. Mpango wa kuondoa umaskini unaweza kusaidia upandaji kanisa ikiwa
Made with FlippingBook Digital Publishing Software