Theolojia Katika Picha
/ 1 9 5
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)
Ufafanuzi • Hakuna ujuzi utakaofundishwa au bidhaa itakayozalishwa kwa sababu tu inathaminiwa na jamii au ina uwezekano wa kuzalisha faida. Ujuzi na bidhaa zote lazima ziende sanjari na malengo ya haki, amani na ukamilifu ambayo ni sifa ya utawala wa ufalme wa Kristo. Ujuzi na njia za uzalishaji zinazodhalilisha utu wa binadamu na bidhaa zinazoendeleza ukosefu wa haki, ukosefu wa usawa, au taabu za kibinadamu hazipaswi kuchukuliwa kuwa zinafaa kwa maendeleo bila kujali kwamba zinakubalika na jamii kwa ujumla. • Lengo la kazi ya maendeleo halipaswi kuwa kuwasaidia watu kupata na kuzalisha rasilimali tu, bali pia kuwasaidia kujitolea kutumia rasilimali hizo kwa ajili ya Ufalme wa Mungu. Kusaidia watu kupata elimu, ujuzi au mali hatimaye hakutakuwa na matokeo wala maana yoyote ikiwa mambo haya hayatawekwa katika utumishi wa Mungu na utumishi wa wengine. Miradi mizuri ya maendeleo itawapa watu fursa ya kumtumikia Mungu si tu kwa kutumia faida za kazi zao bali kupitia kazi zenyewe. Watenda kazi wa maendeleo lazima wafundishe watu kwamba kazi ni fursa ya kumtumikia Mungu na kuwa kielelezo katika hilo (Kol. 3:23-24). Kila moja ya hoja zilizoorodheshwa hapo juu ina sehemu inayoitwa “Maelezo” na sehemu ya “Ufafanuzi.” Hata hivyo, ili andiko hili likamilike hatua moja zaidi inahitajika. Kila ufafanuzi lazima uambatane na vipengele kadhaa vya utendeaji kazi . Vipengele hivi vya utendeaji kazi vinapaswa kuandaliwa na watenda kazi wa maendeleo shambani (eneo la kazi), na kupangwa kwa kuendana na mahitaji mahususi ya hali au mazingira ya eneo husika. Katika kuunda programu hizi, miongozo ifuatayo inapaswa kufuatwa: • Kila huduma ya wenyeji inapaswa kupitia kwa kina sehemu za “Ufafanuzii” na kuamua juu ya hatua mahususi ambazo zitawawezesha kutumia kanuni hizi katika mradi wao mahususi wa maendeleo. • Hatua hizi zinapaswa kuendelezwa kwa njia inayohusisha watu (walengwa) wanaoguswa zaidi na kila mradi wa maendeleo. • Baada ya kukamilika, hatua za utendeaji kazi zinapaswa kuwekwa katika maandishi.
9. Haja ya Kutendea Kazi Hoja
Made with FlippingBook Digital Publishing Software