Theolojia Katika Picha
1 9 4 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)
hili haliwezekani, maandalizi na mafunzo makini yanapaswa kufanyika ili kuhakikisha kwamba kila mtu anaelewa umuhimu na heshima ya kazi husika. Katika baadhi ya matukio inaweza kuwa muhimu kuukabili mfumo wa thamani wa utamaduni fulani ( ona Miller, 1989) lakini hili inapaswa kufanyika kwa umakini na kwa maandalizi ya kutosha na ushirikishwaji wa kina wa walengwa. • Watenda kazi wa maendeleo wanapaswa kuwaandaa walengwa kukabiliana na hali ambazo wanaweza kukutana nazo mahali pa kazi. Watu kutoka katika tamaduni zenye mwelekeo wa kimatukio, kwa mfano, wanahitaji kuelewa utamaduni unaozingatia muda kama ilivyo kwa ulimwengu wa shughuli wa Marekani. Kuwasaidia wafanyakazi kupata ujuzi na taaluma ili waweze kufanikiwa katika jamii pana ni sehemu muhimu ya mchakato wa mafunzo. 8.5 Lengo la maendeleo ni kumtukuza Mungu kupitia ubora na utumishi, si tu kupata faida. Maelezo Katika maadili ya ulimwengu wa shughuli, kiashiria cha juu zaidi cha mafanikio kwa kawaida ni faida ya shughuli au biashara husika. Hata hivyo, kazi ya maendeleo ambayo inaongozwa na maadili ya Ufalme inahusisha maono mapana. Maendeleo yanalenga kusisitiza umuhimu wa kufundisha na kulea watu na utengenezaji wa bidhaa bora inayokidhi mahitaji ya binadamu. Kwa kuwa lengo la juu la juhudi zetu za maendeleo ni kutoa vielelezo bora vya uongozi wa Kikristo na wa kitaaluma, ni lazima tusisitize bila tashwishi faida za nje na pia faida za ndani. Kwa upande mmoja, biashara, kama inataka kudumu, lazima izalishe na faida na iweze kujitegemeza yenyewe. Kwa upande mwingine, ni lazima tujitahidi kujenga wanaume na wanawake waliokomaa kiroho na vile vile walio na mwelekeo thabiti wa kitaaluma na uwezo wa kiufundi. Kutengeneza utajiri si lengo la msingi, ni matokeo ya kujihusisha na biashara kwa jicho la ubora, katika jina la Kristo.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software