Theolojia Katika Picha

/ 1 9 3

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)

Ufafanuzi • Watenda kazi wa maendeleo wanapaswa kuelewa tamaduni na tamaduni ndogo za watu wanaofanya nao kazi . Watenda kazi wa maendeleo wanapaswa, kwanza kabisa, kupata uelewa wa msingi wa asili ya utamaduni wa binadamu na mikakati ya kukuza uhusiano mzuri wa mafunzo katika muktadha wa tamaduni mchananyiko. 7 Wanapaswa kupata ujuzi wa msingi unaohitajika kufanya kazi katika mazingira ya tamaduni mbalimbali (kufahamu lugha, n.k.). Inapendekezwa sana kwa mfanyakazi wa maendeleo kuwa na mshauri ama kutoka katia utamaduni husika wa eneo lake la kazi au ambaye ni mtu mwenye ujuzi wa utamaduni huo, ili kusaidia katika mchakato wa mafunzo. • Mazingira ya kazi yanapaswa kuwa yanayofaa kiutendaji na ya kupendeza yanapotazamwa katika mtazamo wa wafanyakazi au wafanya biashara wa tamaduni husika. Tamaduni zote za wanadamu hutamani mazingira ambayo yanachanganya kufaa kiutendaji na uzuri kimuonekano. Kuna tofauti kubwa, hata hivyo, katika namna ambavyo uzuri (kimuonekano) na kufaa kiutendaji vinafafanuliwa, kupewa kipaumbele na kutumiwa kati ya utamaduni mmoja hadi mwingine. Mazingira ambamo mradi wa maendeleo unafanyika yanapaswa kuzingatia masuala ya kitamaduni. • Watenda kazi wa maendeleo wanapaswa kuwa makini na namna migogoro inavyoshughulikiwa na utamaduni wa watu wanaofanya kazi kati yao. Migogoro ni sehemu isiyoepukika ya kufanya kazi pamoja. Inaweza kuwa fursa nzuri ya ukuaji ikiwa itashughulikiwa kwa njia sahihi. Tofauti za kitamaduni, hata hivyo, zinaweza kuharibu mchakato wa usimamizi wa migogoro. Mfanyikazi wa maendeleo lazima azingatie kwa umakini mitazamo ya kitamaduni kuhusu uwazi/kutokuwa mwazi, aibu/ hatia, ubinafsi/ujima, n.k. na kufanyia maboresho namna yake ya kudhibiti migogoro ili kuzingatia masuala hayo. Lazima pia achukulie kwa uzito jukumu lake la kuandaa watu kutoka katika tamaduni ndogo kufanya kazi ndani ya utamaduni mkuu (unaotawala). • Watenda kazi wa maendeleo wanapaswa kuwa makini na majukumu au kazi ambazo zinachukuliwa kuwa za kudhalilisha katika utamaduni husika . Ingawa kazi zote halali zina thamani mbele za Mungu, tafsiri za kitamaduni za jukumu na hadhi zina nguvu kubwa sana ya kuunda mitazamo. Inapowezekana, ni muhimu kuchagua kazi ambazo hazichukizi katika utamaduni husika. Ikiwa

7 Nyenzo za msingi zinazoweza kusaidia kupata ufahamu kuhusu tamaduni ni pamoja na The

Missionary and Culture (Cornett 1991), Beyond

Culture (Hall 1976), Christianity Confronts Culture (Mayers 1974), Ministering Cross-Culturally (Lingenfelter and Mayers 1986) na Cross-cultural Conflicts: Building Relationships for Effective Ministry (Elmer 1993).

Made with FlippingBook Digital Publishing Software