Theolojia Katika Picha

1 9 2 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)

8.4 Watenda kazi wa maendeleo wanapaswa kuheshimu tofauti za kitamaduni na kujitahidi kuunda mfumo wa mafunzo ambao utawafaa wale wanaowezeshwa. Maelezo Kila utamaduni wa mwanadamu ni “taswira inayowapa watu binafsi katika jamii husika njia ya kutafsiri maisha na kukabiliana nayo. Unawafundisha watu jinsi ya kufikiri, kutenda na kuitikia ipasavyo katika hali yoyote ile. Unaruhusu watu kufanya kazi pamoja kulingana na uelewa wa pamoja wa uhalisia. Hupangilia njia za kufikiri na kutenda katika mifumo ambayo inaweza kurithishwa kwa wengine” (Cornett 1991, 2). Utamaduni huchonga kila aina ya shughuli za kibinadamu kutokana na tabia zinazoonekana (lugha, mavazi, chakula, n.k.) hadi mawazo na mitazamo ya ndani (mifumo ya fikra, tafsiri za uzuri na thamani, nk.). Kuelewa jinsi utamaduni unavyoona uhalisia wa mambo, kile unachothamini, na jinsi unavyofanya kazi ni taarifa za msingi kwa mfanyakazi wa maendeleo. Ingawa tamaduni zote za wanadamu zimeathiriwa na mitazamo ya dhambi, mitazamo na tabia ambazo lazima zikabiliwe na Injili, bado Maandiko yanazitambua na kuziadhimisha tamaduni za wanadamu. Mitume walithibitisha kwamba kuwa Mkristo hakuhitaji kubadili utamaduni wa asili wa mtu (Matendo 15). Maono ya Ufalme wa Mungu tangu Agano la Kale (Mika 4) hadi Agano Jipya (Ufu. 7:9) yanahusisha watu kutoka katika kila taifa, lugha na kabila. Wamishenari, kuanzia na Paulo mwenyewe na kuendelea wameiweka Injili katika muktadha, wakiiweka kweli ya milele katika namna ambazo zingeweza kueleweka na kutumiwa na watu wa tamaduni mbalimbali ( Ona Cornett 1991, 6-9). Watenda kazi wa maendeleo, vivyo hivyo, lazima waheshimu tofauti za kitamaduni na watafute kuweka maelekezo na rasilimali zao katika muktadha wa utamaduni husika ( Ona Elliston, Hoke na Voorhies 1989). Watenda kazi wa maendeleo lazima wawe na nia ya kipekee katika kuyawezesha makundi ambayo yametengwa, kukandamizwa au kupuuzwa na jamii kubwa. Hii itahusisha mara kwa mara kufanya kazi na vikundi au watu binafsi ambao wako tofauti na utamaduni unaotawala. Kazi ya maendeleo itawawezesha ipasavyo wahamiaji, vikundi vya watu wasiokubalika, au watu ambao wameathiriwa na ubaguzi wa rangi au wa kitabaka, ikiwa tu inaelewa na kuheshimu tofauti za kitamaduni za vikundi hivi. Mwisho, watenda kazi wa maendeleo lazima wawaandae watu kuishi na kufanya kazi katika jamii yenye mchanganyiko wa watu na tamaduni. Kujifunza jinsi ya kuwasiliana kwa ufanisi na wateja na wafanyakazi wenza kutoka tamaduni zingine imekuwa sehemu kuu ya mafunzo ya kazi. Ingawa kazi ya maendeleo lazima ianze na muktadha wa kitamaduni wa wale wanaosaidiwa, lazima pia iwawezeshe kuheshimu tamaduni zingine na kufanya kazi kwa ufanisi na mafanikio katika jamii kwa upana wake.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software