Theolojia Katika Picha
/ 1 9 1
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)
8.3 Maendeleo hayatafuti kuwahakikishia watu usawa wa matokeo, bali usawa wa fursa. Maelezo Maendeleo yanazingatia kutoa mazingira ambayo watu wanaweza kujifunza umuhimu wa kazi na taaluma za kazi, kupata ujuzi ambao utaongeza thamani ya kazi zao, na kutumia taaluma na ujuzi wanauopata. Hata hivyo, hakuna jitihada za kibinadamu ambazo hazitegemei nguvu ya kimaadili ya uwezo wetu wa kuchagua, yaani, kuamua ikiwa tutatumia au hatutatumia kikamilifu karama, fursa, na uwezo ambao tumepewa. Kwa sababu ya tofauti za motisha, juhudi na maandalizi, tofauti za mapato haziepukiki na zinapaswa kutarajiwa. Mipango ya maendeleo inapaswa kufundisha na kutuza juhudi. Ufafanuzi • Kila mwanafunzi wa maendeleo (mlengwa) ana jukumu muhimu katika mafanikio yake mwenyewe. Ingawa watendaji wa maendeleo wanaweza kutoa kiasi kikubwa cha utaalam na usaidizi katika kuwezesha jitihada za walengwa za kutengeneza utajiri, sifa nyingi muhimu zinazohitajika kwa ajili ya mafanikio ya kudumu ziko katika mamlaka na maamuzi ya walengwa wenyewe. Bila maono yanayohitajika, nguvu, na kujitolea kufanya kazi kwa muda mrefu wa kutosha ili faida iweze kuonekana, mafanikio hayatatokea. Sifa hizi hazitokani tu na uwepo wa watoa elimu na wawezeshaji wa maendeleo, bali hutokana na ari na imani ya walengwa. Kwa sababu hii, maendeleo hayawezi kuwahakikishia mafanikio wale wote wanaohusika katika mradi fulani. • Uaminifu katika uwakili unapaswa kusababisha kuongezeka kwa wajibu . Miradi yote ya maendeleo inapaswa kuwa na mpango wa kutoa thawabu kwa wale wanaoonyesha uaminifu, kukua kwa ujuzi, na bidii. Haki inadai kwamba kuongezeka kwa juhudi kupelekee ongezeko la thawabu.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software