Theolojia Katika Picha

1 9 0 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)

Ufafanuzi • Vita vya kiroho ni sehemu muhimu ya mchakato wa maendeleo.

Waefeso 6:12 linatukumbusha kwamba “kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.” Kazi ya maendeleo ambayo haitengi kwa makusudi na mara kwa mara muda wa maombi na nidhamu nyingine za kiroho haiwezi kuleta mabadiliko ya kudumu. Watenda kazi wa maendeleo wanapaswa kuwa na mpango wa vita vya kiroho ambao ni lengo muhimu kama mipango kazi yenyewe ya maendeleo. Watenda kazi wa maendeleo wanapaswa pia kutambua kwamba miradi yao itapata mashambulizi ya kiroho. Mkusanyiko wa pesa au nguvu ndani ya mradi unaweza kuwa mianya ya kuingia kwa upotoshaji wa mradi huo licha ya nia yake nzuri. Uhusiano kati ya viongozi na watenda kazi wa mradi wa maendeleo, au kati ya watenda kazi wa maendeleo na wale wanaowafundisha na kuwahudumia (walengwa), unaweza kupotoshwa kupitia migogoro, wivu, kutokuelewana, na tofauti za kitamaduni. Ni lazima kulinda mahusiano binafsi na programu za kitaasisi dhidi ya nguvu za kiroho ambazo zinaweza kuzipotosha au kuziharibu. Hili linahitaji kujizatiti kwa namna endelevu kwa ajili ya vita vya kiroho, na utakatifu binafsi na wa pamoja. 6 • Kazi ya maendeleo inapaswa kupinga mazoea yasiyo ya haki. Watenda kazi wa maendeleo lazima wafundishe watu kuzungumza wazi wazi dhidi ya vitendo visivyo vya haki katika namna zinazoonyesha upendo na haki ya Mungu. Ingawa shirika lisilo la faida lenyewe si jukwaa la utetezi wa kisiasa, lina wajibu wa kuwafundisha watu kuthamini haki na kufanya maamuzi katika muktadha wa maadili. Kazini, wafanyakazi watakabiliwa na ukosefu wa haki katika muktadha binafsi na wa kimfumo na wanapaswa kuzoezwa kuitikia kwa njia inayomheshimu Kristo na maadili ya Ufalme wake. • Jukumu la Kanisa katika maendeleo lisipuuzwe . Andiko la Waefeso 2:14 linasema kwamba ni «Kristo mwenyewe» ambaye ndiye amani yetu na ambaye «amekibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga» kati ya Wayahudi na Wamataifa. Upatanisho umejikita katika nafsi na kazi ya Kristo na hivyo umuhimu wa mwili wa Kristo, Kanisa, hauwezi kupuuzwa. Miradi ya maendeleo ya kimishenari inapaswa kutokana na makanisa imara na kuzalisha makanisa imara.

6 Tazama Thomas McAlpine, Facing the Powers (McAlpine, 1991) kwa maarifa zaidi kuhusu njia ambazo mitazamo ya Wanamageuzi, Anabaptisti, Karismatiki, na Sayansi ya Jamii inatoa mitazamo tofauti na uelewa wa pamoja katika kuelewa na kukabiliana na nguvu za giza.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software