Theolojia Katika Picha
/ 1 8 9
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)
watu kwa ajili ya kuisikia Injili kwa kuishuhudia kweli yake na kuyaishi matokeo yake. • Upatanisho kati ya watu binafsi, matabaka, na tamaduni ni kigezo muhimu. Maendeleo bila shaka yatahusisha njia mpya za kugawana madaraka, kutumia rasilimali, kufanya maamuzi, kutekeleza sera, na kuhusiana na wengine. Kuna haja ya kuvumbua na kuboresha badala ya kuiga tu mifano iliyopo. Ni muhimu sana kuwepo na uwakilishi wa maoni ya watu kutoka matabaka na tamaduni mbalimbali katika kupanga mradi wowote wa maendeleo. • Miradi ya maendeleo lazima izingatie kutopoteza rasilimali na kutoharibu mazingira . Amri ya Mungu kwa wanadamu ni kutambua umiliki wake, na kutonyonya wala kuharibu dunia yake, bali kuihifadhi na kuitunza. Usimamizi unahusisha kutumia rasilimali za dunia ili kumtukuza Mungu na kukidhi mahitaji ya majirani zetu huku tukikumbuka wajibu wetu kwa vizazi vijavyo. Maendeleo lazima yawe endelevu, yaani, yasitumie rasilimali tu bali yaziimarishe pia. Biblia inafafanua mazoea mabaya mbalimbali ya kiadili yanayoweza kusababisha umaskini katika maisha ya watu binafsi (k.m., uvivu, uzembe, kupuuza wajibu, taz. Mit. 6; Mit. 24, n.k.). Hata hivyo, ni wazi pia kwamba umaskini unaweza kusababishwa na mambo makubwa ya kijamii na kiuchumi ambayo yanaleta hali ya uhitaji, dhuluma, na uduni (rej. Isa. 1; Isa. 54, Amosi 4, 5, nk). Hata usomaji wa haraka wa Maandiko unatosha kutusaidia kugundua kwamba katika historia yote ya Biblia manabii walishutumu mazoea fulani ya biashara, siasa, sheria, viwanda, na hata dini ambayo yalichangia kukosekana kwa usawa kati ya makundi mbalimbali ndani ya jamii, na kusababisha ukandamizaji wa watu maskini. Maendeleo yanatafuta kuwa na utendaji wa kinabii kwa kuthibitisha kwamba Mungu anawajali maskini na wahitaji, na hataendelea kuvumilia ukandamizaji wao milele. Maendeleo sio ujinga. Hayahusishi umaskini wote katika jamii na tabia mbaya za mtu binafsi. Kinyume chake, mapambano dhidi ya ukosefu wa haki yanadai kwamba watu watambue uwezekano uliopo wa ushawishi wa nguvu za giza katika mifumo ya wanadamu (1 Yoh. 5:19). 8.2 Maendeleo yanatambua misingi ya kimfumo na kitaasisi inayopelekea uzalishaji wa mali au uwepo wa umaskini. Maelezo
Made with FlippingBook Digital Publishing Software