Theolojia Katika Picha
1 8 8 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)
Haki hutokana na kutambua kwamba vitu vyote ni vyaMungu na vinapaswa kugawanywa kulingana na sifa yake ya ukarimu na kutokuwa na upendeleo. Haki ya Kibiblia inahusu kutenda kwa usawa na kurejesha mahusiano sahihi. Inachukia ukandamizaji, ubaguzi na ukosefu wa usawa kwa sababu inaelewa kwamba matendo ya aina hiyo husababisha kutengana baina ya watu na kati ya watu na Mungu. Maendeleo ambayo yana msingi wa haki ni hatua muhimu kuelekea kurekebisha mahusiano yaliyoharibika kati ya watu binafsi, na baina ya matabaka na tamaduni ambazo zinaweza kuwa na mashaka na nia mbaya dhidi ya matabaka na tamaduni zingine. Kazi ya maendeleo inalenga kuibua na kukuza matendo sahihi na kupelekea mahusiano sahihi. 8.1 Maendeleo yanatokana na ufahamu wa kibiblia wa Mungu kama Muumba na Mtawala wa ulimwengu, jambo ambalo linadai kwamba vitu vyote vipatanishwe ndani yake. Maelezo Mungu amewakabidhi wanadamu wajibu wa kuwa mawakili wa uumbaji wake. Uelewa huu unajidhihirisha katika kujali aina tatu pana za mahusiano: mahusiano na Mungu, mahusiano na wengine, na mahusiano na mazingira ( ona Elliston 1989, Transformation, 176). Ingawa mahusiano haya yalivunjwa kwa kuingia kwa dhambi ulimwenguni, utawala wa ufalme wa Mungu sasa unadai urejesho wake. Maendeleo yanatambua kwamba mpaka hapo utimilifu wa Ufalme wa Kristo utakapodhihirishwa, bila shaka kutakuwa na umaskini, unyonyaji, na taabu inayosababishwa na uharibifu ambo dhambi imeusababisha juu ya maeneo haya matatu ya uhusiano. Uelewa huu haupoozeshi wala kukatisha tamaa maendeleo ya kweli ya Kikristo. Ingawa tunaelewa asili ya uovu wa kimaadili ulimwenguni, maendeleo ya kweli yanatafuta kutoa vielelezo vya haki na upatanisho ambavyo vinaakisi haki ya Ufalme wa Kristo. Ufafanuzi • Maendeleo yana nia ya kuwasogeza watu katika uhusiano sahihi na Mungu . Upatanisho wa kweli kati ya watu unategemea upatanisho wao na Mungu. Ingawa “neema ya kawaida” na “mfano wa Mungu” hutoa msingi kwa kiwango fulani cha upatanisho kati ya watu wote, hatimaye aina ya kina na ya kudumu ya upatanisho inaweza kutokea tu kupitia uhusiano sahihi na Mungu kwa njia ya Kristo. Kwa hiyo, kazi ya maendeleo ina shauku ya kusaidia katika kuwaandaa
8. Kazi ya Maendeleo ya World Impact Inalenga Haki
Made with FlippingBook Digital Publishing Software