Theolojia Katika Picha

/ 1 8 7

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)

7.3 Shughuli za maendeleo zinapaswa kufanyika pasipo lawama. Maelezo

Ukamilifu (ustawi) na utakatifu ni dhana zisizoweza kutenganishwa. Namna ambavyo kazi ya maendeleo inafanyika itakuwa na athari kubwa juu ya uwezo wake wa kuleta mabadiliko. Ili kazi ya maendeleo iweze kuchangia kuleta ukamilifu, uzima na ustawi wa watu ni lazima kuchukua tahadhari maalum kwa ajili ya kudumisha uadilifu katika maneno na matendo. Ufafanuzi • Miradi ya maendeleo inapaswa kudumisha viwango vya juu vya maadili. Ukosefu wa fedha au wafanyakazi wa kutosha na shinikizo la mahitaji ya haraka ya kibinadamu vinaweza kutushawishi «kupindisha mistari» katika namna tunavyoandaa na kusimamia miradi. Jaribu hili lazima lipingwe. Matokeo yetu hayawezi kutenganishwa kiholela na matumizi ya kanuni za uadilifu katika michakato yetu. Miradi ya maendeleo lazima iwe kielelezo kwa serikali, jamii kwa ujumla, na watu wanaohudumiwa kwa kuzingatia viwango vya juu vya maadili ya uendeshaji wa shughuli. • Miradi ya maendeleo lazima ifanye kazi ndani ya mfumo wa sifa yetu ya 501(c)(3) kama taasisi isiyo ya faida. Sheria za Jimbo na za kitaifa zinawekea mipaka mashirika yasiyo ya faida kuwa na uwezo wa kutengeneza mazingira ambapo watu binafsi wanaweza kupokea mali na rasilimali moja kwa moja kutoka kwa mashirika husika. (Hii inazuia watu binafsi ndani na nje ya shirika kutumia vibaya sifa ya taasisi isiyo ya faida kwa manufaa binafsi). Mipango inapowekwa ili kuwawezesha watu na kugawa rasilimali, watenda kazi wa maendeleo lazima wahakikishe kwamba wamejipanga kwa namna ambayo wanaangukia ndani ya miongozo ya kisheria. • Kuvutia wafadhili hakupaswi kuchochea hatia, kuzidisha mahitaji, kuahidi matokeo yasiyo ya kweli, au kudhalilisha utu wa wapokeaji wa misaada . Kuweka katika muhtasari ugumu wa mahitaji na mahusiano ya kibinadamu kuwa wito wa kuvutia wafadhili ni kazi ngumu na yenye changamoto nyingi. Lakini, ni kazi muhimu na ya lazima. Watenda kazi wa maendeleo katika uwanja huo wanapaswa kuchukua jukumu binafsi la kupeleka mahitaji na maono kwa njia sahihi kwa wale wanaohusika katika usambazaji wa nyenzo zinazochapishwa kuhusiana na mradi.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software