Theolojia Katika Picha
1 8 6 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)
Maeneo yote ya uhitaji wa mwanadamu ni muhimu kwa mtenda kazi wa maendeleo. Upendo wa mtenda kazi wa maendeleo kwa watu unapoendelea kusitawishwa kupitia matendo mema, nia yake inapaswa kuwa kwamba watu “wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni” (Mt. 5:16 ). • Watenda kazi wa maendeleo wanapaswa kuwa wanafunzi wa Kristo wanaokomaa ambao wamejiwekeza kikamilifu katika ukuaji endelevu wa kiroho. Jinsi tulivyo (utu na utambulishowetu) ni muhimu zaidi kuliko kile tunachofanya. Ni pale tu wafanya kazi wa maendeleo wanapotafuta kwa bidii kuishi katika pendo la Kristo na kumsikiliza Roho wake, ndipo watakapoweza kuufikisha upendo wake kwa ufanisi kwa wale wanaowahudumia. • Watenda kazi wa maendeleo lazima wapate matunzo kwa ajili ya afya na maendeleo yao ya kimwili, kiakili, kihisia na kiroho . Watenda kazi wa maendeleo wanakabiliwa na changamoto za kipekee katika kushughulikia mahitaji ya kibinadamu. Mara nyingi wanahisi shinikizo fulani kutokana na kusimama katikati, na kuguswa kwa kina na maslahi ya watu mahususi wanaowahudumia, wakati huo huo wakitakiwa kusimama na matakwa ya shirika wanaloliwakilisha (Angalia Hiebert 1989, 83). Kuchoka kwingi kimwili, kihisia au kiroho ni jambo linaloweza kuwatokea. Kwa hiyo, ni muhimu kwamba watenda kazi wa maendeleo watoe muda na umakini wa kutosha katika kudumisha afya zao ili waweze kuendelea kuhudumia ipasavyo mahitaji ya wengine. • Watenda kazi wa maendeleo wanahitaji kupewa mafunzo mahususi katika uinjilisti na ufahamu wa umisheni . Watenda kazi wa maendeleo ya Kikristo kwa kawaida wanaelewa kwamba maendeleo na uinjilisti vinapaswa kufanya kazi kwa ushirikiano, lakini mara nyingi hawana mafunzo ya kutosha ya uinjilisti (Ona Hoke na Voorhies 1989). Watenda kazi wa maendeleo pia wanahitaji kupokea mafunzo ya jumla kuhusu umisheni na usimamizi pamoja na mafunzo wanayopewa kuhusiana na kazi yao mahususi ya maendeleo (Angalia Pickett na Hawthorne 1992, D218-19) kwa kuwa kazi zao nyingi za kila siku zinahitaji uelewa wa taaluma hizi.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software