Theolojia Katika Picha
/ 1 8 5
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)
Ufafanuzi • Watu si vifaa vya kutumia kutimiza malengo.
Maendeleo yanatafuta, kwanza kabisa, kuwaendeleza watu. Hii itahusisha kuwaandaa (na kuwawajibisha) ili waweze kukamilisha kazi. Hata hivyo, kusudi lengwa la msingi la kazi ya maendeleo ni kukua na kustawi kwa mtu, sio kukamilika kwa kazi. • Watu wote katika mchakato wa maendeleo wanapaswa kutumikiana kana kwamba wanamtumikia Kristo mwenyewe . Andiko la Wakolosai 3:23-24 linatukumbusha kwamba kazi yetu hatimaye inaelekezwa kwa Kristo na kutunukiwa na Yeye. Miradi ya maendeleo lazima itekeleze kanuni hii. Hili linadokeza kwamba kazi yetu lazima ifanywe kwa ubora, uadilifu, bidii, upole, upendo na sifa nyingineyo yote inayohitajika kwa ajili ya utumishi ufaao kwa Mungu. • Mienendo ya mahusiano lazima ichukuliwe kwa uzito. Mradi wa maendeleo ambao unaleta matokeo bora na kuwapa watu ujuzi wa soko, lakini una sifa ya mafarakano na kutokuelewana baina ya wafanyakazi wake haujafikia lengo lake. Mleta maendeleo lazima atafute kukuza mahusiano ya kweli mahali pa kazi.
7.2 Shughuli za maendeleo zinapaswa kuakisi kweli ya Injili. Maelezo
1 Yohana 3:18 hutuhimiza tupende si kwa maneno au ulimi tu, “bali kwa tendo na kweli.” Upendo wa Kristo si kwa “nafsi” pekee bali ni upendo kwa mtu katika ujumla wake. Shughuli za maendeleo zinapaswa kumhudumia mtu katika ujumla wake (yaani maeneo yote ya utu wake) na zitumike kama uinjilisti kwa vielelezo. Kazi ya maendeleo inatumika kama ishara ya Ufalme kwa kuwezesha watu, familia, na\au jamii kupata upendo na utunzaji wa Kristo. Hili linamaanisha kwamba watenda kazi wa maendeleo lazima wamjue Kristo kwa karibu na waweze kuakisi upendo wake kwa wengine. Ufafanuzi • Miradi ya maendeleo inaweza kulenga maendeleo ya kiakili, kimwili, kijamii au kiuchumi.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software