Theolojia Katika Picha
1 8 4 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)
• Maendeleo yanapaswa kuepukana na mienendo iliyokithiri ya kuwatawala watu kimabavu kama watoto, kwa upande mmoja, na kuepukana na uendeshaji wa mambo kiholela pasipo mwongozo kwa upande mwingine . Watenda kazi wa maendeleo, kwa ufafanuzi, ni viongozi, na hawawezi kuepuka wajibu wao wa kushauri, kulea, kufundisha na kutoa mwelekeo kwa wale wanaowahudumia. Hata hivyo, kudumisha udhibiti kamili wa kufanya maamuzi hakukuzi mahusiano ya kutegemeana. Ingawa ufuatiliaji wa karibu ni muhimu katika hatua za awali za mafunzo, watenda kazi wa maendeleo lazima watambue haja ya kurekebisha mikakati na ushirikishwaji kwa kuzingatia uwezo na maendeleo endelevu ya wanafunzi. 5 • Miradi inapaswa kuwasaidia walengwa kuchukua udhibiti wa hatima zao wenyewe. Miradi lazima itathminiwe mara kwa mara ili kuhakikisha kwamba haiwafanyi watu kutegemea kuajiriwa kwa muda mrefu na shirika la kimishenari. Lengo ni kuwa na miradi ambayo inawawezesha watu kupata ajira kupitia biashara zilizopo au kuanzisha biashara zao wenyewe. Ukamilifu ( Shalom ) ni hali binafsi na ya kijumuiya yenye amani, utele, wema, uzima, ustawi, na mali. Ukamilifu unatokana na haki (mahusiano mazuri na Mungu na wanadamu), kweli (imani sahihi kuhusu Mungu na mwanadamu), na utakatifu (matendo mema mbele za Mungu na mwanadamu). Shalom ni zawadi ya Mungu na ishara ya uwepo wa Ufalme wake. 7.1 Maendeleo yanapaswa kutengeneza mazingira ambapo uhusiano wa ushirika unaweza kustawi. Maelezo Maendeleo yanayopelekea ukamilifu yanatambua kwamba shughuli za kibinadamu hufanyika katika jamii. Mtandao wa mahusiano unaotokea katika mazingira ya kazi (k.m. mkufunzi na mwanafunzi, mtenda kazi na mtendaka kazi mwenza, n.k.), lazima uakisi maadili yetu kama jamii ya Kikristo.
5 Kwa ufahamu zaidi kuhusu mfumo wa mafunzo wa Hersey Blanchard ambao huzingatia mtindo wa uongozi kwa kuendana na uwezo na mitazamo ya wanafunzi, tazama Leadership Research (Klopfenstein, 1995)
7. Kazi ya Maendeleo ya World Impact Inalenga Ustawi na Ukamilifu
Made with FlippingBook Digital Publishing Software