Theolojia Katika Picha

/ 1 8 3

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)

Vipengele hivi vinapokuwepo, maamuzi mengi yanapaswa kufanywa na watu wenye dhamana ya kutekeleza maamuzi hayo. Maamuzi yote lazima yazingatie muktadha wa ndani na upekee wa watu, mahusiano, na hali za mradi zilizopo. • Mishahara inapaswa kuwa ya haki. Kazi ya maendeleo inapohusisha ajira, mfanyakazi anapaswa kulipwa kwa usawa kulingana na mchango wake katika mafanikio au faida ya mradi. • Programu za mafunzo zijumuishe kufundisha juu ya umuhimu wa uwakili na utoaji. Umuhimu wa watu kutoa kwa Mungu, kwa wengine na kwa jamii yao unapaswa kuwekwa wazi katika mchakato wa maendeleo. Ni muhimu kuimarisha utambulisho wa kila mtu kama mchangiaji au mdau na kusisitiza uhusiano wa asili uliopo kati ya kupokea na kutoa (Luka 6:38). Maendeleo yanasisitiza kuwa kila mtu anapaswa kufundishwa na kuwezeshwa ili kufikia uwezo wake wa kujitegemea na kujiongoza. Kutengeneza au kulea utegemezi kunapunguza hitaji la kina la mwanadamu la kuwa muumba mwenza pamoja na Mungu katika kutumia vipawa vyetu kumheshimu, na kutafuta umuhimu na nafasi yetu ulimwenguni. Utegemezi unaweza kutokea kwa kusababishwa na upande mmoja au mwingine wa uhusiano wa kusaidia watu; mwanzilishi wa programu anaweza kujenga mtazamo na hisia za umuhimu wake mwenyewe, jambo ambalo linaweza kusababisha utegemezi, au mlengwa anaweza kukataa kwa urahisi kuendelea kukua kuelekea kutegemeana na kina. Utegemezi huchafua mchakato wa maendeleo ya kweli kwa kujenga uhusiano usiofaa ambao unaharibu jitihada na motisha binafsi ya mlengwa wa maendeleo. Ufafanuzi • Ni lazima kuwataka walengwa kuonyesha juhudi. Kanuni ya msingi ya kidole gumba ni “Usiwafanyie watu kile wanachoweza kujifanyia – hata kama ina maana kwamba mradi (au mafunzo) utaenda polepole” (Hoke na Voorhies 1989, 224). Kuwafanyia mengi kupita kiasi watu wanaosaidiwa ni kuwanyima fursa ya kujifunza kutokana na makosa yao. Utegemezi, hata unapotokana na roho ya ukarimu na huruma, bila shaka huzuia ukuaji wa wale ambao wameathiriwa nao. 6.3 Kazi ya maendeleo lazima ilenge kuondoa mwelekeo wa utegemezi. Maelezo

Made with FlippingBook Digital Publishing Software