Theolojia Katika Picha
1 8 2 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)
Ufafanuzi: • Hakuna kitu kinachoweza kumwepusha mfanyakazi, kiongozi, au mtaalamu na ulazima wa uwajibikaji binafsi na hatari zinazoweza kujitokeza kutokana na kutokuwajibika. Wafanyakazi Wakristo hawana kinga ya moja kwa moja itakayowazuia kuingia katika mazoea mabaya ya uvivu, uzembe, usimamizi mbaya, na pupa, na hawataepushwa na matokeo ya tabia na mienendo kama hiyo. • Ni lengo la msingi la maendeleo kukuza ukomavu wa kila mtu anayehusika katika mchakato na shughuli hizo. Inachukuliwa kuwa mtu anayepevuka atazidi kuwa na sifa ya maono (kujiwekea malengo, matarajio na vipaumbele vya maisha), uwajibikaji (kutenda kulingana na malengo, matarajio na vipaumbele hivyo kwa motisha, uvumilivu na uadilifu), na hekima (kuongezeka kwa ustadi, ufahamu na uwezo wa kupambanua na kufanya kile kinachofaa kwake mwenyewe na kwa wengine). Watu wanaokomaa wanapaswa kuhama kutoka katika hali ya utegemezi kuelekea uhuru, kutoka katika hali ya kutokuwa na shughuli (kukaa tu) kuelekea katika maisha yenye shughuli na wajibu, kutoka uwezo mdogo hadi uwezo mkubwa, kutoka kwenye masilahi finyu hadi masilahi mapana, kutoka katika ubinafsi hadi uungwana (tabia ya kufikiria wengine), kutoka katika ujinga kuelekea kuelimika, kutoka katika hali ya kujikinai hadi kujikubali, kutoka katika kujitenga kuelekea kwenye tabia na mtazamo wa ushirikiano, kutoka katika kuiga kuelekea uhalisia na kutoka katika ugumu wa kimtazamo (kutotaka kubadilika) kuelekea uvumilivu na kuchukuliana (Klopfenstein 1993, 95-96). • Maamuzi yanakuwa na ufanisi zaidi yakifanyika karibu zaidi na wale walioathirika. Sera na taratibu za kitaifa zipo ili: » Kutoa mfumo wa kufanya maamuzi kwa ufanisi. » Kufafanua maadili na madhumuni ya pamoja kama taifa. » Kuhakikisha kuna haki na usawa kati ya watu na miradi katika maeneo mengi tofauti. » Kuleta uwajibikaji unaolinda uadilifu. Kukiwa na maamuzi makini ndani ya jamii maana yake kuna watu waliokomaa na ambao wana dhamira ya dhati ya kusimamia madhumuni haya ya pamoja na kuhakikisha kwamba kuna mawasiliano ya wazi baina ya watu wanaohusika.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software