Theolojia Katika Picha
/ 1 8 1
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)
• Mahali pa kazi panapaswa kutumika kama jumuiya inayojali. Ingawa mazingira mengi ya kazi yana sifa ya kutojali utu, maendeleo ya Kikristo yanapaswa kujitahidi kuunda mfumo bora wa mahusiano baina ya walengwa na wafanyakazi. Watenda kazi wa maendeleo na wale wanaoshiriki katika mradi wa maendeleo lazima watengeneze mienendo inayokuza mazoea ya kujaliana pasipo kujalisha changamoto za mradi husika. 6.2 Maendeleo yanapaswa kuwawezesha watu kuwajibika kikamilifu kwa ajili ya maisha yao wenyewe na kujali mahitaji ya wengine . Maelezo Maendeleo yanatokea kutokana na imani kwamba kazi zote ni za heshima. Mungu ameamuru kwamba wanadamu wapate riziki zao kwa uadilifu na ubora. Agizo hili la kazi ya mtu binafsi limejikita katika amri ya awali ya Mungu waliyopewa wanadamu wakati wa uumbaji, na inaendelea na kuthibitishwa tena katika mafundisho ya mitume. Ingawa Mungu anataka kwamba watu wake wawe wakarimu kwa wenye uhitaji na wageni (2 Kor. 9), Mungu vivyo hivyo amewaamuru watu wote wafanye kazi kwa unyoofu kwa mikono yao wenyewe (1 The.4), na zaidi ameagiza kwamba wale wanaokataa kufanya kazi wanapaswa kunyimwa misaada, yaani, “ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi asile chakula” (taz. 2 The.3:10). Maendeleo yanakataa dhana ya kwamba kutengeneza ukwasi ni uovu kwa asili. Mtazamo kama huo ni mwepesi (hauna uzito wala mantiki) na utashindwa kusimama mbele ya wazo la kibiblia la uwakili wa Kikristo. Maendeleo yanalenga kutengeneza utele, lakini kamwe si kwa ajili ya faida ya ubinafsi au uchoyo na tamaa. Badala yake, maendeleo yanachukulia kwa uzito takwa la kibiblia kwamba tufanye kazi, si tu kukidhi mahitaji yetu wenyewe, bali ili kutokana na utele ambao Mungu anatukirimia tuweze kutumia mali na rasilimali zetu kukidhi mahitaji ya wengine, hasa wale ambao ni ndugu na dada zetu katika mwili wa Kristo (rej. Efe. 4; 2 Kor. 8; Gal. 6). Kiwango cha kibiblia ni kwamba wale walioiba kabla ya kuingia katika Ufalme wasiibe tena, bali wafanye kazi za heshima kwa utulivu na uadilifu, ili wawe na rasilimali za kutosha kukidhi mahitaji yao wenyewe, na kuwa na mali za kutosha kuwajali wengine. Maendeleo si tu kwamba yanalenga kuwaheshimu wahitaji kwa kuhakikisha kwamba wanaweza kushiriki katika haki ya msingi ya binadamu ya kufanya kazi, pia yanawapa changamoto ya kumwamini Mwenyezi Mungu kuwatimiziamahitaji yao kwa njia ya kazi za heshima zinazowawezesha kuwa wafadhili wao wenyewe na wa wengine.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software