Theolojia Katika Picha
1 8 0 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Kuwawezesha Watu kwa ajili ya Uhuru, Ustawi na Haki (muendelezo)
6.1 Maendeleo yanawathibitishia wanadamu kuwa ni wa thamani na wa pekee machoni pa Mungu, na kuamini kwamba wamepewa uwezo wa kipekee na
Mungu. Maelezo
Kama viumbe walioumbwa kwa mfano wa Mungu, kila mtu bila kujali cheo au mahali alipo, anastahili hadhi na heshima. Watu wanapaswa kuthaminiwa, kutunzwa, na kufadhiliwa kwa sababu ya thamani na upekee wao wa asili mbele za Mungu. Maendeleo yenye msingi wa Kibiblia hayatawanyonya watu kwa ajili ya malengo ya kiuchumi au kuwachukulia watu kama vyombo vya kutumikishwa kufikia matokeo fulani, badala yake yatawathamini kama walengwa wakuu wa maendeleo husika, wanaostahili kupendwa na kuheshimiwa kwa sababu ya thamani waliyonayo mbele za Mungu. Ufafanuzi • Watu wanapaswa kupewa kipaumbele katika kila nyanja ya maendeleo . Maendeleo yanapaswa kuchangia katika uwezekano wa kujitosheleza, yanapaswa kuimarisha ubora wa maisha, na kuhimiza uwakili mzuri miongoni Kwa maskini, maisha katika jamii za mijini yamejaa usumbufu, shida, na aibu. Wahitaji kila siku hupitia matusi na udhalili katika jamii tajiri kwa sababu ya umaskini wao. Mara nyingi wanashutumiwa kwa utovu wa kimaadili, wanakabiliwa na urasimu kandamizi na kuhukumiwa kwamba wanasababisha umaskini wao wenyewe kwa kukosa uwezo au kukosa motisha. Maendeleo yanapaswa kuzingatia kwa umakini mkubwa jumbe hizi zinazotolewa kwa wahitaji katika jamii zetu. Yanatambua kwamba maskini ni walengwa wa huruma, wema na habari njema za Mungu, waliochaguliwa kuwa matajiri katika imani na warithi wa Ufalme wa Mungu (Yakobo 2:5). Kupitia kazi na mahusiano mahususi, maendeleo yanatafuta kudhihirisha namna ambavyo Mungu katika haki na ukarimu wake anawapenda na kuwajali maskini. Misaada isiyotolewa kwa msingi wa heshima ya kweli inaweza kuwadhalilisha maskini kwa urahisi. Kwa hiyo, msaada unaotolewa kwa wahitaji lazima uthibitishe utu na heshima yao. Kitu chochote katika mchakato wa maendeleo ambacho kinapunguza thamani na umuhimu wa watu kwa sababu ya umaskini ni dhambi na ni chenye madhara kwa ustawi wa pande zote, wale wanaotoa msaada na wale wanaopokea. mwa wale wanaoshiriki katika programu husika. • Kuheshimiana ndio msingi wa maendeleo ya kweli .
Made with FlippingBook Digital Publishing Software